Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi
Mwanamke
mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi
karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka
minane bila wanaume hao wawili kujitambua.
Hayo
yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya baada ya Mwanamke
huyo kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa miaka
miwili eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani
Mwashilindi mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Juliana
alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne
asubuhi alipokuwa akielekea soko la Sido kwenye shughuli zake za
biashara na kutoa taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa na baadaye kituo
kikuu kati na kufunguliwa jalada la wizi wa mtoto namba MB/RB/9384/2014
ambapo juhudi za kumtafuta zilifanikiwa baada ya taarifa kutolewa Kituo
cha Radio cha Bomba FM Mbeya ndipo alipojisalimisha mwenyewe akiwa na
mtoto Zalida Rogers(2).
Hata
hivyo katika hali ya mshangao Biton alifika katika kituo cha Polisi
Kati akiwa na Cheti cha kuzaliwa na kadi ya kliniki ambapo kinaonesha
mtoto Zalida kuzaliwa kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa na kuonesha
kuzaliwa 18/08/2012 wazazi wakiwa ni Juliana Josia na Biton Mwashilindi.
Biton
alidai mbele ya Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi kuwa Juliana ni
mpenzi wake kwa muda wa miaka nane na kwamba walikuwa wakikutana katika
nyumba ya kulala wageni kila alipomhitaji na walikuwa wakipanga katika
nyumba hiyo kwa siku saba kila wanapokutana hali ilyofanya watu
wanaosikiliza tukio hilo kituo cha Polisi kushikwa na butwaa akiwemo
mume halali Rogers Halinga na mke wa Biton ambaye alimtunza mtoto kwa
siku nne.
Akijieleza
kwa kujiamini Biton alidai kuwa hata mtaji wa biashara alimpatia yeye
na hata wazazi wake Biton walioko Itaka Mbozi walimtambua mtoto Zalida
na kwamba jina la mtoto alipewa na ndugu zake na hata aliowahi kuugua
alikwenda Itaka Mbozi na kukaa kwa wazazi wa Biton kwa zaidi ya juma
moja.
Kwa
upande wa Rogers yeye alisema mtoto Zalida ni wa kwake na kwamba
aliondoka kwao akiwana na ujauzito wa miezi mitano na kwamba yeye alijua
kukorofishana kwao kulitokana na hali ya ujauzito na alikaa kwamba
mkewe Juliana alikaa kwao kwa miezi sita na alipojifungua alirejea kwake
na aliohitaji kupata maendeleo ya mtoto mkewe alidai kuwa kadi ya
kliniki imepotea.
Kikao
hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa kiliahirishwa na Mkuu wa Polisi
Wilaya ya Mbeya kwa kumshikilia Biton kwa kosa la kutorosha mtoto na
kesi ya ugoni na kuwa atafikishwa mahakamani pindi upelelezi
utakapokamilika huku Rogers akikabidhiwa mkewe na mtoto kwa minjili ya
kwenda kuyajenga huko nyumbani kwao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa
wilaya ya Mbarali.
Baba
mzazi wa Rogers Mzee Jason Halinga alisema alishangazwa na kitendo
kilichofanwya na mwanamke huyo ambapo alidai kuwa mwanae alioa kihalali
na kufuata mila zote na kulipa mahari lakini alishangazwa na kitendo cha
wazazi wa Juliana kushindwa kuonesha ushirikiano hali inayoashiria
kujua kile kilichokuwa kinafanywa na mtoto wao.
Biton
alifika kituo cha Polisi akiwa na mkewe wa ndoa ambapo naye hakufahamu
kuwa mumewe anaishi na mke mwingine nje ya ndoa na kwamba mtoto Zalida
alipoletwa kwake hakuambiwa chochote kile na kwamba ameishi kwenye
mateso ya ndoa kwa muda wa miaka nane huku akifanyiwa vitendo vya
kikatili na mumewe ikwa pamoja na kuambulia kipigo mara kwa mara.
Baadhi
ya ndugu wa Rogers walioneshwa kukerwa na baadhi ya Askari wa ngazi
juu katika Dawati la Jinsia Kituoni hapo ambao walonesha kutojali suala
hili huku wakitioa maneno ya kejeli hali inayotia dosari utendaji kazi
wa Dawati hilo na kwamba lipo kibiashara zaidi na si huduma kama ilivyo
sera ya Jeshi la Polisi.
Hata
hivyo hawakusita kuwapongeza Askari wa Kiume walionesha juhudi hata
kufanikwa kupatikana kwa mtoto Zalida na Biton pamoja na rafiki yake.
Katika
sakata hili kama si juhudi za Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed
Msangi kuingila kati basi mtoto Zalida asingeweza kupatikana kama baadhi
ya watoto waliotoweka maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambao
hawajapatikana mpaka sasa ambapo wananchi wamelalamikia Kituo Kikuu cha
Kati kwa kutochukua hatua za haraka za kukomesha vitendo vya ukatili wa
Kijinsia na baadhi kuamua kumalizana wenyewe mitaani vikiwemo vitendo
vya ubakaji ambavyo vimeshamiri mkoani Mbeya.
Hatima
ya ndoa ya Rogers na Juliana itajulikana baada ya mazungumzo
yatayofanyika kwa Mzee Jason Halinga nyumbani kwake Ishungu Kata ya
Ruiwa hivi karibuni kikao kitakutaniha pande mbili za wazai ili kufikia
muafaka katika sakata la aina yake na kwamba hata kubainika kwa sula
hili ni kutokana na Juliana kufumwa na mwanaume mwingine katika chumba
ambacho Biton alikuwa awe na Juliana ndipo alipoamua kulipiza kisasi kwa
kutorosha mtoto.
Na Mbeya yetu
|