My God! Mama
aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini
Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya
kujifungua kiumbe wa ajabu.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo
ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00
usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani
Mvomero mkoani hapa.
Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu.
Katika tukio hilo, ilielezwa kwamba Swaumu alijifungua kiumbe huyo wa ajabu anayedaiwa kuwa na mkia mrefu huku akiwa hana miguu.
Ilidaiwa kwamba baada ya kutokea kwa
tukio hilo, baadhi ya ndugu walishikwa na taharuki kubwa huku wengine
wakitoa taarifa kwa mwanahabari wetu ambaye alifunga safari kutoka mjini
Morogoro na kuwasili kwenye kituo hicho cha afya majira ya saa 12:00
asubuhi.
Katika mahojiano maalum na gazeti hili
juu ya tukio hilo, nesi wa zamu aliyekutwa kituoni hapo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Consolatha alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimpokea Swaumu majira ya saa 1:00 usiku akilalamika kuwa na uchungu
wa kujifungua.
“Nilimpa kitanda. Saa 8:00 usiku,
uchungu ulizidi nikampeleka leba ambako alijifungua kiumbe huyo mwenye
jinsi ya kiume. “Baada ya kujifungua na kumuona kiumbe huyu wa ajabu,
nilitimua mbio usiku huo kwa woga na kwenda kuamsha manesi wenzangu
wanoishi kota za kituo hiki cha afya.
“Nimefanya kazi hii ya ukunga na kuzalisha wazazi zaidi ya 50 lakini sijawahi kukutana na tukio kama hili.”
Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha:
Kwa upande wake mganga mkuu wa kituo hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Beatrice alikuwa na haya ya kusema juu ya tukio hilo la kusikitisha:
“Kimsingi si kiumbe ila ni mtoto ambaye
awali tulipomcheki mzazi tulibaini ana kichwa kikubwa na alishafia
tumboni zaidi ya siku tatu.
“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”
“Amezaliwa akiwa na miezi nane tumboni. Tulichokifanya ni kuokoa maisha ya mama jambo ambalo tumefanikiwa.”
Akizungumza kwa tabu na mwanahabari
wetu, Swaumu alisema: “Hii ni mimba yangu ya tatu, ya kwanza iliharibika
tumboni, ya pili nilifanikiwa kuzaa salama mwanangu Maimuna.
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.”
“Hii ya tatu ndiyo nimejifungua kitu hiki cha ajabu.”
Alipoulizwa kwa nini aliondoka Dar
ambako ndiko kwenye hospitali kubwa na kwenda kujifungulia kijiji akijua
ana matatizo ya uzazi, mama huyo alisema:
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.”
“Siku za kujifungua zilipokaribia mume wangu Abdallah aliniambia nije kujifungulia kwa bibi yangu Halima, kwa bahati mbaya ndiyo yametokea haya.”
Kwa upande wake shangazi wa Swaumu
aliyekutwa akimhudumia alisema: “Yameshatokea ya kutokea, tunamshukuru
Mungu na tunajiandaa kumchukua mjukuu wetu tukamzike.”
MAAJABU..!! MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU
Reviewed by Unknown
on
1:37:00 AM
Rating: