AIBUU...KIGAUNI KIFUPI CHAMUUMBUA DIDA..UTAMU WOTE NJE...PICHA ZOTE HAPA






Prizenta asiyekaukiwa matukio wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar, Khadija Shaibu ‘Dida’.

Tukio hilo lililoibua gumzo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye shughuli ya ya kuzaliwa (birthday) ya shosti wake ambaye ni mtangazaji wa Kipindi cha Mcharuko wa Pwani kupitia Kituo cha Redio Planet FM cha mkoani hapa, Warda Makongwa.


Katika tukio hilo lililochukua nafasi kwenye Ukumbi wa White House mjini hapa, Dida alishuhudiwa akizama ukumbini humo akiwa mpole na mwenye kujificha kufuatia kuvaa kihasara lakini kadiri muda ulivyosonga ndivyo alivyokuwa akichangamka


Khadija Shaibu ‘Dida’ akijificha sura yake asipigwe picha na papalazi wetu. Kuna wakati mtangazaji huyo alinyanyuka na kwenda kumvaa mwimbaji nyota wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Amigo kisha akamgeuza na kumkatia mauno kabla ya kutaka kushikana na MC Chuma aliyekuwa anaongoza shughuli hiyo.

“Mh! Lakini naye Dida jamani kigauni gani kile kinaonesha hadi mambo ya ndani!” alisikika mmoja wa mashabiki wa Dida aliyekuwa ukumbini hapo.

Ili kuziba watu midomo, Dida alizama kwenye waleti yake akaibuka na ‘Misimbazi’ ambayo alimmwagia Warda na kuibua minong’ono kuwa yupo njema kimkwanja.

Kama hiyo haitosh i, mwanamama huyo alimfuata Meneja wa Planet FM, Anthony Muhando ‘Babu Bomba’ kisha akamkatia nyonga, jambo lililowashangaza wengihuku wengine wakipaza sauti wakisema ‘huyo ndo Dida wa…’ (hawakumalizia Dida wa nani).

Mwanahabari wetu alipomfuata Dida kujua kulikoni kuvaa kihasara na kucharuka kiasi hicho, bidada huyo hakutaka kutoa ushirikian
AIBUU...KIGAUNI KIFUPI CHAMUUMBUA DIDA..UTAMU WOTE NJE...PICHA ZOTE HAPA AIBUU...KIGAUNI KIFUPI CHAMUUMBUA DIDA..UTAMU WOTE NJE...PICHA ZOTE HAPA Reviewed by Unknown on 4:48:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.