AMINI AJIONDOA THT, AAGWA KWA NDEREMO


Amini Mwinyimkuu akiongea mbele ya wageni waalikwa na waandishi wa habari kwenye sherehe hiyo ya kuagwa.
Mkurugenzi wa THT, Ruge Mutahaba (kushoto), akipokea tuzo ya shukurani kutoka kwa Amini.
Mhasibu wa THT,  Rehema Mwenda (kushoto), akipokea cheti cha shukurani kutoka kwa Amini muda mfupi kabla ya sherehe fupi ya kuagwa.
Mmoja wa walimu wa THT, Richard Mangustino (kulia), akipokea cheti cha shukurani kutoka kwa Amini.
Amini akiwa katika pozi na mkewe.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Makomando, Mucky (kushoto), akipozi na Amini.
Mwigizaji wa kipindi cha Mahusiano kutoka THT, Mwemba Mwijaku (kulia), akipozi na Amini.
MSANII wa Bongo Fleva zao la nyumba ya kukuza vipaji Tanzania ‘THT’, Amini Mwinyimkuu jana jioni alifanyiwa hafla fupi ya kuagwa na uongozi wa THT.
Tukio hilo lilifanyika ndani ya ofisi hizo zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, karibu kabisa na Viwanja vya Leaders Club ambapo Amini alipata muda wa kuwaaga baadhi ya wasanii wenzake na uongozi kwa ujumla wa THT.
Akizungumza kwenye hafla hiyo alisema kwamba ameamua kuondoka mikononi mwa chuo hicho baada ya kupata kampuni mpya ya BME CO LTD,ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ingawa atabaki kushiriki kwenye kazi maalum za THT pindi atakapohitajika.
Kupitia hafla hiyo, Amini aliweza kutoa vyeti na tuzo za shukurani kwa baadhi ya viongozi wake wa juu na walimu wote waliomsaidia kukuza kipaji chake wakati akiingia kwenye chuo hicho cha muziki.
AMINI AJIONDOA THT, AAGWA KWA NDEREMO AMINI AJIONDOA THT, AAGWA KWA NDEREMO Reviewed by Unknown on 7:43:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.