Mtoto wa miaka (5) mkazi wa Kijiji cha Kabuhima Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita amefanyiwa ukatili wa kinyama baada ya kubakwa na jirani yao.
Mtuhumiwa
anayedaiwa kufanya kitendo hicho cha kikatili inadaiwa kuwa alimkuta
mtoto huyo anacheza mlangoni kwao akiwa hajavalishwa nguo ya ndani na
wazazi wake jambo lililpelekea kufanya ukatili huo.
Akizungumuza
na mwandishi wa habari hizi mzazi wa mtoto huyo, Benjamini Juma akiwa
kituo cha afya cha Uyovu akisubiri vipimo na matibabu ya mtoto wake
(jina tunalo) alimtaja mtu anayedaiwa kufanya kitendo hicho kuwa ni Juma
Manjariwa anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 28 ambaye wanaishi nyumba
moja ya kupanga
Alisema
mwanae alikutwa na mkasa huo wakati yeye akiwa ndani amepumzika baada
ya chakula cha mchana saa 7:37 mchana ambapo mama wa mtoto alikuwa
amekwenda kusuka kwa jirani.
Alisema
aliamua kutoka nje na kukuta kijana huyo anatoka nje na kuanza
kukimbia, huku mtoto akitokwa na damu nyingi sehemu zake za siri.
Mganga Mkuu wa kituo cha afya Kata ya Uyovu, Joshua Mazingo alisema,“Mimi
nikiwa safarini nilipokea taarifa za mtoto huyo ambaye alifikishwa
kwenye kituo cha afya kupimwa kisha kukutwa na mbegu za kiume na kwamba
tunaendelea kumpima vipimo vingine kubaini kama ameambukizwa magonjwa
mengine ya zinaa.”
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kubakwa kwa mtoto na kwamba polisi tayari wamemkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kubakwa kwa mtoto na kwamba polisi tayari wamemkamata mtuhumiwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA JIRANI YAKE WA MIAKA MITANO ALIKUWA AKICHEZA UCHI MLANGONI KWAKE
Reviewed by Unknown
on
11:48:00 PM
Rating: