HAIJAKAA sawasawa!
Siku chache baada ya Sitti Abbas Mtemvu (25) kujivua taji la Miss
Tanzania 2014 kwa madai ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu umri
wake, wadau wamemwangushia uwajibikaji mwingine wakimtaka avue mataji
mengine mawili.
Baadhi ya wadau wa sanaa waliozungumza
na Risasi Mchanganyiko Jumatatu iliyopita jijini Dar walisema kama kweli
Sitti ana dhamira safi ya kukwepa kusakamwa basi ni bora kwake akavua
na mataji ya Miss Chang’ombe na Miss Temeke ambayo ndiyo yaliyompa
tiketi ya kwenda kambi ya Miss Tanzania na kushinda.
Wadau hao walisema kuwa, sheria za Miss
Tanzania zinaanzia vitongojini, wilaya, mikoa, kanda na hatimaye taifa
kwa hiyo kama skendo ya kudanganya umri imemla mpaka akaamua
kujisalimisha, basi bado hana sifa za kuwa Miss Chang’ombe na Miss
Temeke wa mwaka 2014.
“Kwanza kabisa nasema Sitti hajavua taji
la Miss Tanzania kwa sababu ya kusakamwa na vyombo vya habari kuhusu
kudanganya umri bali ni kweli amedanganya, anajijua.
“Kama angekuwa hajadanganya, kwa nini
asitoe paspoti yake inayomwonesha ana umri wa miaka 23? Mambo yalimfika
shingoni ndiyo maana. Anachotakiwa ni kuvua taji la Miss Chang’ombe na
Miss Temeke mwaka huu,” alisema Ismail Chandu, mkazi wa Temeke jijini
Dar.
Shindano la Miss Temeke 2014 lilifanyika
Agosti 22, mwaka huu kwenye Ukumbi wa TCC Club, Chang’ombe jijini Dar
ambapo Sitti Mtemvu aliibuka kidedea akifuatiwa na Salama Saleh
(anayetakiwa kushika nafasi ya kwanza) na nafasi ya tatu ilitwaliwa na
Neema Mollely.
Novemba 5, mwaka huu, Sitti Mtemvu
aliiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania inayoongozwa na Hashim
Lundenga akisema ameamua kwa hiyari yake kuvua taji hilo.Sitti alifikia
uamuzi huo baada ya kuandamwa na skendo ya kudanganya umri wakati
akigombea taji hilo.
SITTI MTEMVU KUVUA TAJI LA TEMEKE, CHANG’OMBE
Reviewed by Unknown
on
11:53:00 PM
Rating: