KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
WAZIRI MKUU
- Kamati imesema imejiridhisha pasipo
mashaka kuwa, Waziri Mkuu, alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na
mchakato mzima wa kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya ESCROW.
-Kamati, kwa kuzingatia kielelezo namba
22, inathibitisha bila shaka kwamba, Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo
hili vizuri na kwamba aliridhia muamala huu ufanyike. Ndiyo maana katika
maelezo yake ya
Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.
Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za Escrow hazikuwa fedha za Umma.
- Ripoti yasema ni jambo la kushangaza
kuona kwamba, jambo kubwa na zito kama hili lingeweza kufanyika bila ya
mamlaka za juu, hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu.
-Yaongeza kuwa kwa uzito na unyeti wa
jambo hili, vyovyote vile, Waziri Mkuu anapaswa kuwajibika kwa kauli
zake na kwa kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba ipasavyo, ili
kurejesha imani ya wananchi
kwa serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.
kwa serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema.
MWANASHERIA MKUU
-Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki Kuu ya Tanzania
kuhusiana na hukumu ya Jaji Utamwa J. Kwa kutumia madaraka yake vibaya,
Mwanasheria Mkuu
wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 107
na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu.
wa Serikali aliagiza kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21 bilioni isilipwe 107
na hivyo kuikosesha Serikali mapato adhimu.
- Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua
na kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa kwamba mgogoro uliopelekea
kufunguliwa kwa Akaunti ya
ESCROW ulikuwa ni mgogoro wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati ya TANESCO na IPTL. Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha
afikishwe mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

Ads by InfoAd Options
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
- Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa
Nishati na Madini amekuwa, mara kwa mara, akilipotosha Bunge tukufu na
Taifa kwa ujumla kuhusiana na Fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW kwamba
ndani ya
fedha hizo hakukuwa na fedha za umma. Hata mtu wa kawaida angeweza kujua kwamba washirika wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na masharti ya kutoka kwa fedha hizo kwenye akaunti ni yapi
kwa mujibu wa Mkataba wa uendeshaji wa akaunti hiyo.

-Hata hivyo, katika hali ya kushangaza,
aidha kwa makusudi ama kwa sababu anazozijua vizuri zaidi mwenyewe,
Waziri wa Nishati ananukuliwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge, Kwa
nguvu
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba wa Escrow.
Ads by InfoAd Options
-Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa
Nishati na Madini ndiye alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana
Harbinder Singh Sethi na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya
Umma; na
pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.
pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.
-Iwapo Waziri wa Nishati na Madini
angetimiza wajibu wake ipasavyo, Fedha za Tegeta ESCROW zisingelipwa kwa
watu wasiohusika, na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea kama
kodi za VAT,
Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 30.
Capital Gain Tax na Ushuru wa Stempu ambazo ni sawa na takribani shilingi bilioni 30.
-Kamati inapendekeza kuwa Mamlaka yake
ya uteuzi itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini kutokana sababu
hizo zilizoelezwa.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri
wa Nishati na Madini alisema uongo Bungeni kwa kutamka kauli ambazo
zilizokuwa na lengo la kupotosha umma kuhusu akaunti ya Tegeta ESCROW
ikiwemo kutoa
kauli ambazo zingeweza kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.
kauli ambazo zingeweza kusababisha Nchi kuingia kwenye mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.
Ads by InfoAd Options
-Kamati inapendekeza kuwa Naibu Waziri
wa Nishati na Madini achukuliwe hatua kali za kinidhamu ikiwemo
kutenguliwa uteuzi wake. Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri huyu
afikishwe mbele ya
Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya Bunge lako tukufu.
Kamati ya Bunge ya Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa wabunge wengine kuhusiana na kauli wanazotoa ndani ya Bunge lako tukufu.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
-Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini aliingia makubaliano ya kutoa fedha
katika Akaunti ya Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu kuwa
maamuzi ya hukumu ya ICSID 2 yalikuwa bado kutolewa na hivyo kusababisha
fedha kutolewa bila kukokotoa upya gharama za ‘capacity charges’, jambo
ambalo limesababisha kupoteza fedha za umma.
-Vile vile, Kamati imebaini kuwa, Katibu
Mkuu hakufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kujiridhisha uhalali
wa Kampuni ya Mechmar kuuzwa kwa Piperlink na baadaye kuuzwa kwa PAP, na
hivyo kusababisha fedha za akaunti ya Tegeta ESCROW kulipwa kwa
asiyestahili na kinyume cha Mkataba wa akaunti ya Escrow.
-Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, pengine kwa uzembe wake ama kwa kukusudia kwa sababu
anazozijua yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.
-Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali
ya juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo, kushindwa kujiridhisha kama
masharti ya Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu cha 90(2)
yalitekelezwa. Kifungu hicho kimsingi kinaitaka mamlaka ya ‘approval’’
ya uhamishaji wa Makampuni kutotambua Kampuni mpaka kwanza kodi za
uhamishaji ziwe zimelipwa na hati za malipo ya kodi zimetolewa na
mamlaka ya kodi.
-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa
Katibu Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU wamfikishe mahakamani mara
moja, kwa kuikosesha Serikali Mapato, matumizi mabaya ya ofisi na
kusaidia utakatishaji wa fedha haramu.
KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW
Reviewed by Unknown
on
11:32:00 AM
Rating: