WAKATI sakata
la kuchukuliwa kwa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Tegeta
Escrow likiendelea kuwa gumzo la sasa la mjini, sura mpya imeanza
kujitokeza kwa watu zaidi wanaohusishwa na kugawiwa salio kutajwa, licha
ya waliotajwa awali kuendelea kubakia katika orodha.
Kashfa hiyo iliibuliwa kwa mara ya
kwanza na mbunge wa Kigoma Kusini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David
Kafulila katika kikao cha Bunge lililopita, kitu ambacho kilipingwa kwa
nguvu kubwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Hata hivyo, kadiri siku zinavyokwenda
hali imeonekana kuwa ni ngumu kwa vigogo wa serikali kwani wanaonekana
kama wameshikwa pabaya na wengi wametajwa kuhusika kwa njia moja au
nyingine.
Ukiacha Werema, Muhongo na Eliakim Maswi kutajwa kunufaika na uchotwaji wa fedha hizo zilizokuwa Benki Kuu, wengine wanaodaiwa kupata mgao huo ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndullu.

4Aidha
vigogo wengine wengi, wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, nao
wanatajwa kuhusishwa na ukwapuaji wa fedha hizo kutokana na nyadhifa
zao.
Lakini wakati Bunge hilo likianza vikao vyake vya wiki hii, Spika wa Bunge, Anne Makinda, naye alitajwa bungeni na Mbunge wa Mkanyageni kwa tiketi ya CUF, Habib Mnyaa kuwa anadaiwa kupewa mgao wa dola milioni moja za Marekani.

Kana kwamba haitoshi, Mbunge wa Kigoma
Kaskazini, Zitto Kabwe, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Hesabu za Serikali, katika kijarida maalum kilichochapishwa kumchafua
kilichosambazwa Dodoma, naye anatajwa kuchukua mlungula kutoka kampuni
inayohusishwa na sakata hilo ya PAP.
Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kutunza fedha ambazo Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania (Tanesco) zilipaswa kuilipa kampuni ya kufua umeme wa
IPTL kwa kuiuzia nishati hiyo.
Hiyo ilitokana na shirika hilo la umma,
kushtaki katika mahakama ya kibiashara ikilalamikia bei kubwa iliyotozwa
na IPTL na kusababisha kufunguliwa kwa akaunti hiyo ili fedha hizo
ziwekwe huko hadi muafaka baina ya pande hizo mbili utakapopatikana.
Hata hivyo, kabla ya muafaka huo kupatikana, wajanja walikwenda na kuzichukua fedha hizo ambazo sasa zinawatokea puani
ESCROW NDIYO HABARI YA MJINI
Reviewed by Unknown
on
9:24:00 PM
Rating: