Meninah Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutoa Mimba ya Diamond Platnumz


Mwanamuziki Hot Sexy hapa Bongo, Meninah Atick ameifungukia ishu ya kuchoropoa mimba ya msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na kusema hajawahi kubeba mimba ya staa huyo na wala katika maisha yake hajawahi kufanya kitendo hicho.

“Jamani mimi ni mdogo, kwanza kwa nini watu wanapenda kunibebesha vitu vikubwa, mimi sijawahi kubeba wala kuchoropoa mimba katika maisha yangu,” alisema msichana huyo.

Meninah alienda mbele zaidi na kusema maneno hayo yanaweza kuwapandisha hasira wapenzi wa Diamond na kumjengea nao chuki, wakati ukweli ni kwamba hajawahi kutoka na msanii huyo mwenye historia ya kutoka na wasichana wengi.
GPL
Meninah Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutoa Mimba ya Diamond Platnumz Meninah Afunguka Kuhusu Tetesi za Kutoa Mimba ya Diamond Platnumz Reviewed by Unknown on 11:56:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.