Baadhi
ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa
kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza
baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono. (Picha na Elizabeth Kilindi)
Ads by TheFreeHD-Sports TV 1.1Ad Options
Baadhi
ya majeruhi waliolipukiwa na baruti jana wakati wakivua samaki kwa
kutumia baruti katika Kisiwa cha Karange tarafa ya Pongwe wakiwa
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza
baadhi ya viungo vikiwemo macho na mikono.
Baadhi
ya majeruhi waliolipukiwa na barutiwakiwa wamelazwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo vikiwemo macho
na mikono.
Mmoja wa majeruhi waliolipukiwa na baruti wakiwa wamelazwa katika
Hospitali ya Rufaa ya Bombo huku wakiwa wamepoteza baadhi ya viungo
vikiwemo macho na mikono.
NA ELIZABETH KILINDI, TANGA
Wakazi wawili wa kata ya Tangasisi tarafa ya Pongwe wilayani Tanga wamejeruhiwa vibaya viungo mbalimbali vya mwili kwa kulipukiwa na baruti wakati wakivua kwa kutumia dhana za uvuvi haramu kwenye kisiwa cha Karange.
Tukio hilo limetokea mnamo Novemba 12 mwaka huu majira ya saa nane mchana katika kisiwa ambapo majeruhi hao wakiwa kwenye ngalawa yenye namab za usajili TTA 315 wakati wakijianda kutegesha baruti hizo ndipo zilipowalipukia.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Freisse Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja majeruhi hao kuwa ni Hamis Omari ambaye amekatika mkono wa kulia na ameumia jicho la kulia,huku majeruhi mwingine Adamu Selemani amekatika mikoni yote miwili, pamoja na kupoteza macho yote mawili.
“Hali ya majeruhi wote wawili ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya bombo ni mbaya hii inaonyesha ni kwa kiasi gani uvuvi haramu ulivyo na madhara makubwa kwa jamii pamoja na viumbe wa baharini “alisema Kamanda Kashai.
Hata hivyo kamanda Kashai alitumia fursha hiyo kuwa taka wakazi
wanaoishi maeneo ya bahari kutoa taarifa ya wavuvi wanaojihusisha na uvuvi haramu ili kuweza kuwachukulia hatua mapema kabla ya kutokea kwa madhara zaidi.
WAVUVI HARAMU WAPOTEZA MIKONO, MACHO BAADA YA KULIPUKIWA NA MABOMU YAO WAKATI WAKIVUA.
Reviewed by Unknown
on
6:43:00 AM
Rating: