UPEPO mbaya
unaendelea kuvuma ndani ya Klabu ya Bongo Movie Unity! Safari hii
umewakumba mastaa wakubwa klabuni hapo, Devotha Mbaga, Aunt Ezekiel na
Jennifer Kyaka ‘Odama’ ambao wanadaiwa kutimuliwa kundini kwa sababu ya
kujiweka karibu na mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Steven Mengere
‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozama
katika kikao kilichofanyika juzikati, uongozi ambao ulibaki madarakani
kundini baada ya Steve kujiuzulu, ulifanya tathmini upya ya memba
waliobaki kisha kuwachuja hadi kubaki na wasanii 20 pekee wenye sifa.
“Wamewaengua baadhi ya wasanii ambao
wameona hawana sifa ya kubaki kundini, miongoni mwao ni Devotha, Aunt na
Odama. Wamesema wanahitaji mastaa wenye msimamo siyo kujipendekeza
upande wa Steve, siku si nyingi watayaanika majina ya wenye sifa za
kubaki kundini,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu’
kuwa, wasanii walioenguliwa ni wanachama hai lakini si wanachama wenye
msimamo na baadhi yao wameonesha udhaifu wa kuwa karibu na Steve Nyerere
ambaye sasa anafanya harakati zake peke yake.
Baada ya habari hizo kutua katika rada
ya Ijumaa, mapaparazi wetu waliwaendea hewani mastaa hao wakubwa
waliodaiwa kufukuzwa, mambo yalikuwa hivi:
Devotha: Mimi ndiyo kwanza nakusikia
wewe siku zote nipo nyumbani sijui hata habari za kikao hicho na sielewi
wameniengua vipi wakati mimi ni mwanachama hai na ni miongoni mwa
waanzilishi toka tulipokuwa watu saba, lakini kama wameamua hivyo sawa
kwani siyo kwamba ukitoka ndiyo mwisho wa maisha.
Odama: Hakuna kitu kama hicho,
wanaoenguliwa ni viongozi siyo wanachama, watanienguaje bila kunipa
taarifa? Kwanza ndiyo nasikia sijui chochote ndiyo napata taarifa kutoka
kwako.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.
Kwa upande wa Aunt Ezekiel, simu yake iliita bila kupokelewa.
HALI SI SHWALI BONGO MOVIE..!! AUNT, ODAMA WATIMULIWA BONGO MOVIE
Reviewed by Unknown
on
10:48:00 PM
Rating: