OMMY DIMPOZ AITWA MSHAMBA WA KIGOMA SOMA HAPA

“WANANIITA mshamba wa Kimanyema ila poa tu!”Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema baadhi ya mashabiki wake wanamuita mshamba wa Kimanyema, lakini hilo halimsumbui na wala halimpi presha.

Nyota huyo anayetamba na wimbo ‘Ndagushima’, amesema hawezi kuacha kufurahia kupiga picha nyingi iwezekanavyo anavyosafiri nje ya nchi kwani ni kumbukumbu kwake na pia ni kitu alichokiota kwa muda mrefu.

“Eti wanasema mshamba wa Kimanyema kapata vihela vyake eti kaenda shopingi, nifanyaje sasa na ni kitu ninachokipenda, sitaacha kutupia picha nikiwa nje au ndani ya nchi kwa kuwa ni kitu ninachokipenda na nadhani wengi wanapenda kwani ni sehemu ya kufurahia maisha,” alisema Ommy Dimpoz.

Msanii huyo amekuwa katika ziara ya wiki mbili sasa katika nchi mbalimbali ambapo kesho Jumamosi, atatumbuiza katika Ukumbi wa La Bodega huko Ufaransa baada ya shoo iliyofanyika wiki iliyopita katika mji wa Rotterdam, Uholanzi.
OMMY DIMPOZ AITWA MSHAMBA WA KIGOMA SOMA HAPA OMMY DIMPOZ AITWA MSHAMBA WA KIGOMA SOMA HAPA Reviewed by Unknown on 10:29:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.