AUNTY EZEKIEL AANGUA KILIO ‘LOCATION

DIVA wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel hivi karibuni alijikuta akiangua kilio alipokuwa eneo la kuigiza ‘location’ pande za Kijichi jijini Dar baada ya kusumbuliwa na jino ambapo alishindwa kuvumilia maumivu.
Diva wa Filamu za Kibongo, Aunty Ezekiel.
Akizungumza  na Amani baada ya kupatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Aviation, Aunty alisema kuwa  alijikuta uvumilivu unamshinda na kuangua kilio kwani kila alipojaribu kufanya kazi alishindwa.
“Huwezi amini sikupenda hata kuongea na watu, jino naliheshimu sana kwani maumivu yake kama hayajakufika unaweza kuona mtu  anajifanyisha,” alisema Aunty.
Baada ya tukio hilo, Aunty aliyekuwa amejichimbia kwenye kambi ya William Mtitu amesitisha zoezi la kupiga picha hadi hali yake itakapokuwa nzuri.
AUNTY EZEKIEL AANGUA KILIO ‘LOCATION AUNTY EZEKIEL AANGUA KILIO ‘LOCATION Reviewed by Unknown on 1:40:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.