MTOTO
mmoja wa miaka 9 (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa darasa
la pili katika Shule ya Msingi Manda iliyopo Kijiji cha Mtimbira,
wilayani Ulanga, Morogoro wiki iliyopita usiku wa manane anadaiwa
kukutwa darasani akiwa na hirizi kubwa kiunoni.Mwananchi akionesha Hirizi iliyofungwa kiunoni mwa mtoto wa miaka tisa (jina linahifadhiwa).
Tukio hilo lilitokea katika moja ya majengo ya Shule ya Msingi Mazoezi Kigurunyembe ya mjini humo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililoshuhudiwa pia na mwandishi wetu, lilijiri Alhamisi iliyopita ambapo mara baada ya kuonekana darasani humo, baadhi ya wananchi walianza kumpa kichapo wakidai kuwa yeye ni mwanga.

Dogo huyo alinusurika kifo kutoka kwa
wananchi hao wa Kigurunyembe waliokuwa na hasira kali baada ya mmoja wa
walimu kuwatuliza na kufanikiwa kumuokoa mwanafunzi huyo na kwenda
kumficha kwenye ofisi ya walimu ya shule hiyo.Hirizi nyekundu ikiwa kiunoni mwa mtoto huyo.
Akihojiwa na Uwazi mwalimu huyo aliyejitambulishwa kwa jina la Zuhura Khatibu alikuwa na haya ya kusema:
“ Wiki hii mimi ni mwalimu wa zamu nilipofika shuleni nikawashuhudiwa wananchi wakimshushia kichapo mtoto huyo, kama mzazi niliumia sana nikawauliza kwa nini wanampiga wakadai eti ni mwanga ameanguka hapa shule usiku, sisi tulipigwa butwaa. Nilimuoka na kumficha ofisini,” alisema Zuhura.

Akizungumza na mwandishi wetu,
mwanafunzi huyo alidai kuwa alitokea Mtimbira kwa ndege ya kichawi,
anatumiwa na wanga na kwamba alipofika pale shuleni wenzake
walimdondosha akaamua kuingia darasani.
Alipoulizwa alikuwa anaelekea wapi usiku
huo, alidai walikuwa wakienda Kihonda kwa baba yake anayefanya biashara
ya mbogamboga. Alipopekuliwa alikutwa na hirizi kubwa yenye rangi
nyekundu kwenye mkanda wa suruali yake, alipoulizwa ilikuwa ya nini
alisema alifungwa ili kumlinda.Mwalimu Zuhura Khatibu akimpeleka mtoto huyo kituoni.
Baada ya mahojiano hayo,walimu hao
walimkabidhi mwandishi wetu mwanafunzi huyo ambapo waliongozana na
Mwalimu Zuhura hadi Kituo cha Polisi Morogoro kwenye dawati la jinsia na
watoto.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Sophia Ngosso alimpokea mtoto huyo na kufungua taarifa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha polisi jalada namba MOR/RB/12659/014.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Sophia Ngosso alimpokea mtoto huyo na kufungua taarifa kwenye kitabu cha kumbukumbu cha polisi jalada namba MOR/RB/12659/014.
Baadaye iligundulika kuwa mtoto huyo
alikuwa anatafutwa na baba yake aitwaye Clarence Kandira ambaye alifika
pale polisi baada ya kupigiwa simu ambapo alimtambua mwanaye na kuangua
kilio na kusema:Baba wa mtoto huyo kushoto, Clarence Kandira akimshukuru msamaria mwema (Zuhura Khatibu).
“Huyu mtoto anasoma darasa la pili
Mtimbira na ana matatizo ya ugonjwa, (hakuutaja), tukiwa nyumbani
Kihonga alipotea katika mazingira ya kutatanisha na hii ni mara ya pili,
mara ya kwanza alipotea hivihivi na kuokotwa kwenye Mto Kilombero akiwa
ndani ya mtumbwi.”
Alipoulizwa kwa nini amemfunga hirizi,
Kandira alidai kuwa haikuwa hirizi bali ni alama yake inayomsaidia
kuonekana kirahisi anapopotea. Afande Sophia alimsainisha Kandira na
kumkabidhi mtoto wake akaondoka naye.
UCHAWI..!! MWANAFUNZI AKUTWA NA HIRIZI DARASANI
Reviewed by Unknown
on
11:36:00 PM
Rating: