Kama
hukusikiliza ama kuangalia kikao cha Bunge leo Novemba 10, moja ya
mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na suala kukosekana kwa dawa katika
Hospitali kutokana na bohari kuu kusitisha huduma ya kusambaza dawa
pamoja na matibabu ya Rais Dkt. Kikwete Marekani.
“..
Kutokana na Serikali kudaiwa bilioni 102 na bohari ya madawa MSD hali
ya Hospitali zetu ni mbaya sana.. wagonjwa wanaendelea kuteseka na
maradhi, madawa hamna.. wanawake wanakufa, watoto wanateseka.. huku sisi
waheshimiwa wabunge tukiendelea kukaa humu tukila viyoyozi’
‘kwa
taarifa tulizonazo Mheshimiwa Rais yupo nje kaenda kuchekiwa afya
yake.. Ili tuwatendee haki Watanzania waliotuweka katika bunge hili na
tuweze kuokoa maisha yao naomba bunge lako liahirishe shughuli
zinazoendelea tuweze kujadii jambo hili kwanza.. tulipatie ufumbuzi kwa
maslahi ya Watanzania.. na kwa maana hiyo naomba kutoa hoja na
waheshimiwa wabunge naomba mniunge mkono..” – Rukia Ramadhani, mbunge viti maalum CUF.
Mbunge Ally Kessy akajibu hoja hiyo;- “..Wabunge
wangapi wa upinzani tayari wameshawahi kwenda India mara sita.. Kwa
majina nawajua tena wa CUF wamekwenda India kutibiwa mara tatu mara nne
leo mnazungumzia habari ya Rais kwenda kutibiwa Marekani, aende kutibiwa
wapi Zanzibar? Acheni mambo yenu hayo..”
Naibu Spika wa Bunge akafunga mjadala huo;- “..Waheshimiwa
wabunge ningewaomba sana kuhusiana na masuala ya wagonjwa wetu
mbalimbali wawe ni wabunge.. Awe ni mheshimiwa Rais na wanatibiwa wapi..
Naliomba jambo hili tuliache litatuharibia hali ya hewa bila sababu
jamani.. Nawaombeni sana hilo nimelitoa katika utaratibu na kwenye
hansard tulifute jamani..”- Job Ndugai.
MATIBABU YA RAIS NCHINI MAREKANI LATUA BUNGENI
Reviewed by Unknown
on
10:56:00 PM
Rating: