Polisi mjini Nairobi wamewakamata watu
100 katika msako baada ya mwanamke mwingine kuvuliwa nguo katika mtaa wa
mabanda wa Kayole mjini Nairobi.
Inadaiwa mwanamke huyo alikuwa amevalia nguo zisizo za heshima.
Naibu kamanda wa polisi mjini Nairobi Moses Ombati, amaenukuliwa akisema wengi wa waliokamatwa walikuwa wanaume walevi.
Bwana Ombati aliongeza kusema kwamba,
mwanamke huyo alishambuliwa katika mtaa wa Kayole Jumatatu jioni na
kwamba polisi wanaendelea na msako.
Mnamo Jumatatu mamia ya wanawake
waliandamana katika barabara za katikati mwa mji kulaani kitendo cha
kumvua nguo mwanamke mwingine mapema mwezi huu mjini Nairobi.
Wanawake hao waliandamana kufuatia wito
kwenye mitandao ya kijamii chini ya kauli mbiu #MyDressMyChoice yaani
vazi langu uamuzi wangu au nitavaa nitakachojiamulia mwenyewe.
Waandamanaji hao wakiwemo wanawake
mashuhuri, wanasiasa na wanaharakati waliandamana hadi katika kituo cha
mabasi ambako mwanamke wa kwanza alidaiwa kuvuliwa mavazi yake kwa madai
alikuwa amevalia 'Mini Skirt'
Wakamatwa kwa Kumvua Nguo mwanamke Hadharani Kenya
Reviewed by Unknown
on
12:23:00 AM
Rating: