Mwimbaji wa zamani wa Twanga Pepeta, Hamis Kayumbu 'Amigolas' enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI wa zamani wa Bendi ya
African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’
amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kulazwa Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili kwa siku kadhaa.
Amigo
alilazwa Muhimbili kwa matatizo ya moyo ambapo taratibu za kufanyiwa
upasuaji zilikuwa zikiandaliwa lakini mauti yakamkuta kabla ya lolote
kufanyika.
Mwimbaji huyu ambaye hadi anafariki, alikuwa mtumishi wa bendi ya Ruvu Stars inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Amigo alikuwa mmoja wa wanamuziki
waasisi wa Twanga Pepeta, akaitumikia kwa uaminifu mkubwa kwa miaka
mingi kabla ya mwanzoni mwa mwaka huu yeye na wenzake kadhaa kuanzisha
Super Stars Band ambayo baadae ikachukuliwa na JKT na kuwa Ruvu Stars
Band.
Akiwa Twanga Amigo akajijengea umaarufu
wa aina yake na kuwa kama moja ya nembo ya bendi, katika utumishi wake
uliotukuka ndani bendi hiyo, akafanikiwa kutunga wimbo mmoja 'AMINATA'
ambao ulikamata chati kwa miaka mingi tangu ulivyorekodiwa mwaka 2003.
Kufariki kwa Amigo ni pengo kubwa kwa Ruvu Stars hasa kutokana na ukweli kuwa yeye ndiye alikuwa
‘injinia’ wa mipango yote kuanzia Super Stars hadi Ruvu.
Kabla ya Twanga Pepeta, Amigo aliitumikia pia bendi ya Bicco Stars chini ya Kinguti System.
Kabla ya Twanga Pepeta, Amigo aliitumikia pia bendi ya Bicco Stars chini ya Kinguti System.
Msiba uko nyumbani kwa mama mzazi wa
marehemu Mburahati jijini Dar es Salaam jirani kabisa na Shule ya Msingi
Mianzini na taratibu za mazishi zinasubiri ndugu na jamaa kutoka Tabora
na Kigoma.
MSIBA!! AMIGOLAS WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA
Reviewed by Unknown
on
11:32:00 PM
Rating: