Sakata la mke kuishi na waume wawili
limechukua sura mpya baada ya kikao cha ndugu wa mume halali, Rogers
Halinga kuketi kikao katika Kijiji cha Ishungu, Kata ya Ruiwa Mbarali,
mkoani Mbeya na kumtaka Biton Mwashilindi kufanya mazungumzo nao kabla
hawajafungua madai ya ugoni mahakamani na kudai fidia.
Kikao hicho kizito kilichofanyika
nyumbani kwa baba mzazi wa Rogers, mzee Jason Halinga (95), Novemba mosi
mwaka huu na kuhudhuriwa na ndugu lukuki nia ilikuwa kumsikiza mke wa
Rogers, Juliana (22) ili abainishe ukweli juu ya mtoto aliyezua utata
kuwa ni wa nani baina ya mumewe (Rogers) na Biton Mwashilindi.
Mwanamke huyo akijikanganya mara kadhaa
katika kikao hicho akidai mtoto huyo ni wa Rogers, kwani aliondoka
baada ya kutokea mabishano na mumewe akiwa na ujauzito wa miezi minne
ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na Biton hadi siku anajifungua
mwaka 2012 akiwa mikononi mwa Biton na aliamua kumwandikisha mtoto
katika kadi ya kliniki kuwa baba yake ni Biton.
Kutokana na kauli hiyo, ndugu wa Rogers
walikuja juu na kumtaka Juliana atamke wazi mtoto ni wa nani ndipo
alijibu kuwa mtoto ni wa Biton Mwashilindi, ambapo alimkabidhi mtoto
huyo mwishoni mwa Oktoba kwa hiari yake na wala hakuporwa kama alivyotoa
taarifa polisi.
Kauli hiyo ya Juliana iliwafanya ndugu
wa mume kupiga simu kwa mzazi wa Juliana anayeishi Lwanjilo wilayani
Chunya kujua mustakabali wa kauli ya mtoto wao kwani ilidaiwa kuwa Biton
aliwahi kwenda huko kujitambulisha kuwa yeye anaishi na mtoto wao kwa
kuwa hakujua kuwa Juliana aliwahi kuolewa kwani alidai kuwa yeye ni
mwanafunzi wa VETA Mbeya.
Baba mzazi wa Juliana, Hosea Mwalukasa
alipopigiwa simu alidai kuwa ni kweli Biton alifika kwake lakini
hakumpokea kwa kuwa alidai kuwa Juliana ni mke halali wa Rogers Halinga,
akawaambia kuwa kama amezaa na Juliana amefanya kosa na kwamba atatozwa
faini ya ugoni kwani mwanaye hakuwahi kupewa talaka na Halinga.
Baada ya mvutano wa muda mrefu kikao
kiliamua kuwa endapo Biton anadai kuwa mtoto aliyezaliwa na Juliana
aliyefahamika kwa jina la Zalida Biton (2) ni wake basi alipe fidia ya
kuzaa na mke wa mtu kiasi cha shilingi milioni kumi au n’gombe saba ili
aweze kumkomboa mtoto wake na kwamba Juliana bado ni mke halali wa
Rogers.
Kwa upande wake Biton alidai kuwa hayuko
tayari kulipa faini hiyo kwa sababu alikabidhiwa mtoto kihalali na
Jeshi la Polisi Oktoba 31, mwaka huu katika Kituo Kikuu cha Kati mbele
ya maafisa wa polisi na kwamba hana kesi ya kujibu na anasubiri mtoto
afikishe umri wa miaka saba ndipo amchukue.
“Baadhi ya wadau wamelilalamikia Jeshi
la Polisi Tanzania kwa kuamua masuala ya kisheria katika vituo vya
polisi badala ya kufikisha katika mamlaka za kisheria kama mahakama.
Uamuzi uliotolewa umesababisha tatizo kuwa zito,” alisema ndugu wa
Rogers aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Amedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa kipimo cha DNA bado hakijatatua mgogoro huo na kwamba suluhu katika ndoa hiyo ni kitendawili kisicho na majibu.
Amedai kitendo cha kukabidhiwa mtoto Biton bila kuchukuliwa kipimo cha DNA bado hakijatatua mgogoro huo na kwamba suluhu katika ndoa hiyo ni kitendawili kisicho na majibu.
CHUNGU YA NDOA..!! MKE ANAYEISHI NA WAUME WAWILI MAPYA YAIBUKA
Reviewed by Unknown
on
10:50:00 PM
Rating: