Pichani ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka akikagua mabehewa mapya leo jijin Dar es Salaam |
NA Karoli Vinsent
Serikali
ya Rais Jakaya Kikwete imedhamilia kuliboresha Shirika la Reli ya kati
TRL ili liweze kujiendesha lenyewe na kuacha kutegemea bajeti ya
Serikali kwenye mipango yak,baada ya leo kampuni hiyo imepokea Mabehewa
50 ya kubebea makasha (Containres), ikiwa ni sehemu ya mradi wa serikali
wa ununuzi wa mabehewa mapya 274 kutoka nchini India.
Ads by InfoAd Options
Kupokelewa
kwa mabehewa hayo, kunatarajia kuongeza kasi ya utoaji wa makasha ya
mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwa njia ya reli kwenda nchi
jirani za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda na
kutimiza malengo ya Big result yaani matokea makubwa sasa.
Akipokea Mabehewa hayo leo Kwenye bandari ya Jijini Dar es Salaa na
kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja v, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Uchukuzi, Shaaban Mwinjaka, alisema serikali inaendelea kutekeleza
miradi 12 kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN), yenye lengo la
kuimarisha huduma ya usafirishaji kwa njia ya reli.
Hapa ndipo Mahebewa hayo yakiwasili leo Jijin Dar es Salaam kwenye bandari |
Alisema
serikali imeshalipa zaidi ya bilioni 45 ikiwa ni gharama za ununuzi wa
mabehewa 274 ambayo ni wastani wa milioni 166 kwa kila behewa.
Ads by InfoAd Options
Vilevile Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa , lengo la serikali ni
kuiwezesha TRL kusafirisha mizigo tani milioni 1.5 kwa mwaka na
kuiwezesha kampuni hiyo kujiendesha kwa faida.
Vilevile
akatabainisha kuwa, baada ya kukamilika kwa mradi huo kutapunguza
uharibifu wa barabara kutokana na mizigo mingi kusafirishwa kwa njia ya
barabara.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Mhandisi Kipallo Kisamfu,
alisema katika mabehewa 274 yaliyokwisha nunuliwa na serikali yatakuwa
ya aina tatu tofauti.
Alizitaja
ainia hizo kuwa ni mabehewa ya kubebea makasha, mizigo kichele na
mafuta ambapo ifikapo mwezi Februali mwakani, mabehewa yote yatakuwa
yameshawasili nchini.
Mwezi
Julai mwaka 2011, serikali iliamua kuiendesha TRL baada ya mwekezaji
kutoka kampuni ya RITES ya India kubainika kushindwa kuiendesha kampuni
hiyo kama ilivyotarajiwa.
HABARI NJEMA JIJINI LEO-MABEHEWA MAPYA YAWASILI NCHINI,SASA TRL KUWA YA KISASA-SOMA HAPA KUJUA
Reviewed by Unknown
on
12:14:00 PM
Rating: