Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi ya Filbert Bayi

Moto mkubwa umeteketeza majengo ya Shule ya msingi Filbert Bayi na kisha kusambaa na kuteketeza mabweni yote ya Wanafunzi pamoja na madarasa.
Mwenyekiti wa shule hiyo Filbert Bayi amesema moto huo ulianza saa nane usiku katika bweni la wanafunzi wa kike na kisha kusambaa shule nzima kutokana na gari za zimamoto kuchelewa kufika mapema.

Hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa wala kudhurika kutokana na moto huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna mwandamizi wa Polisi Litrichi Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili juu ya chanzo cha moto huo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bonyeza play kusikiliza taarifa iliyoripotiwa na televisheni ya TBC 1 kuhusu ajali hiyo.

Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi ya Filbert Bayi Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi ya Filbert Bayi Reviewed by Unknown on 7:46:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.