BETHIDEI YA MTOTO, MKE WA MTITU, DUDE AMKATISHA MAUNO MKEWE

Kazi ipo! Taarifa ikufikie kwamba kutoka kwenye bonge la pati la bethidei ya mtoto na mke wa mwigizaji, William Mtitu, staa wa Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amejikuta akimkatisha mauno mkewe, Eva hadharani kitendo kilichozua minong’ono mingi baada ya mwanamama huyo kufanya kweli hadi jamaa akamwambia yatosha.
Mke wa mwigizaji, William Mtitu, Yovitha akiwa na mwanaye Jane.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri nyumbani kwa Mtitu, Kigogo jijini Dar ambapo Dude alikuwa Master of Ceremony ‘MC’ wakati mke wa Mtitu, Yovitha na mwanaye Jane walizaliwa tarehe inayofanana ya Oktoba 31.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, William Mtitu akiwa na mwanayeJane.
Katika sherehe hiyo iliyojaa kufuru ya fedha na vituko vya mastaa, makundi mbalimbali yalipanda jukwaani na kutoa burudani ya kufa mtu.Awali Dude alianza kwa kuitambulisha ngoma yake mpya ya Kijijini kwa Bibi ambapo aliachia mistari mikali na kuwapagawisha mashabiki wake kwa jinsi alivyokuwa ‘akirap’ kisha kuiongoza vizuri shughuli hiyo.
Mshereshaji  wa siku hiyo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ akimuomba mkewe, Eva akate mauno.
Ulipofika muda wa kukata mayenu ndipo Dude akamwita Eva na kumwambia akate mauno mbele ya kadamnasi ambapo naye alifanya kweli hadi akashangiliwa kabla ya Dude kumkataza kwa madai kuwa ana shughuli nyingine nzito usiku huo.
Eva akikata mauno bila kupepesa macho.
Hata hivyo, Mtitu alionesha kutisha kwa zawadi kubwa aliyomzawadia mwanaye baada ya kutakiwa kutangaza hadharani ambapo aliinadi nyumba wanayoishi kuwa ndiyo zawadi pekee aliyomwandalia mtoto wao kwani yeye na mkewe hawana muda mrefu duniani huku akificha umri wa mkewe lakini mwanaye alikuwa anatimiza umri wa mwaka mmoja.
Mshereheshaji ,'Dude' akionekana kama ni mwenye kuguna na kuchukua uamuzi wa  kuzuia zoezi la mke (Eva) kukata mauno.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali huku washkaji zake Mtitu wa Bongo Movie wakitoa hudhuru na kuwakilishwa na wachache kwa sababu walikuwa safarini.
BETHIDEI YA MTOTO, MKE WA MTITU, DUDE AMKATISHA MAUNO MKEWE BETHIDEI YA MTOTO, MKE WA MTITU, DUDE AMKATISHA MAUNO MKEWE Reviewed by Unknown on 10:58:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.