MIUJIZI YA KARNE: SHEKH SHARIF KHAMIS WA TANZANIA AONYESHA MIUJIZA NDANI YA MELI ..MANAHODHA PAMOJA NA ABIRIA WADUWAA
Shekh Sharif Khamis hapa ndipo alipowaacha watu midomo wazi na mshangao baada ya kuendesha Meli wakati hajawahi kusomea urubani.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma wakiwa kwenye muhadhara kumsikiliza miujiza ya uponyaji wa dua za Shekh Sharif Khamis.
Na Sharifa Abdalah- Bukavu Kongo
Ukisikia
hizi habari kwenye radio unaweza usiamini unaweza ukadhani ni
kichekesho ama hadithi lakini ni kweli yametokea, kijana wa kitanzania
Shekh Sharif Khamis ambae kadri anavyokuwa kiumri ndipo anazidi kufanya
miujiza ya kipekee na ya kuogopesha.
Akiongea na Maskanibongotz mwandishi wetu aliyeko mji wa Bukavu Shekh
Sharifu ambae kabla ya kutua nchini Kongo alikuwa nchi ya Uturki
alikokuwa amepewa mwaliko na Serikali ya huko kwa ajili ya kwenda
kufanya dua na huko nako alifanya maajabu.
Hata
hivyo kwenye tukio hilo la kuendesha meli ilikuwa wakati wakiwa ndani
ya Meli wakitokea mji wa Goma kwenda Bukavu ndipo kijana huyo
alipomwambia nahodha wa meli hiyo kuwa anaweza kuendesha mtambo huo huku
mamia ya watu wakishuhudia palitokea mabishano makubwa huku manahodha
mbalimbali wakimwambia hawezi kuendesha meli hiyo kwa vile kama hajawahi
kusomea uderva hawezi kufanya kitu kama hicho.
Baada
ya mabishano ya muda mrefu nahodha wa meli hiyo iliyofahamika kwa jina
la MV Emmanul alipompa nafasi Shekh huyo na katika hali isiyokuwa ya
kawaida kijana huyo alianza kusukuma mtambo huo huku kila mtu akipigwa
na butwaa kwa tukio hilo na aliendesha kwa muda mrefu hadi kufika mji wa
Bukavu na kutia nanga.
Kufuatia
tukio hilo mamia ya watu walimuogopa Mungu kwa maajabu. hiyo huku
manahodha wakisema huo ulikuwa ni maajabu. mkubwa na wengine wakishindwa
kuamini kama kijana huyo ni binadamu wa kawaida ama ni maajabu.
Hata
hivyo wananchi wa Kongo wamemuomba Shekh Sharif kuwafikishia shukrani
zao kwa Mh Jakaya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwasaidia kwa kupeleka
Majeshi nchini huko mwao.
MIUJIZI YA KARNE: SHEKH SHARIF KHAMIS WA TANZANIA AONYESHA MIUJIZA NDANI YA MELI ..MANAHODHA PAMOJA NA ABIRIA WADUWAA
Reviewed by Unknown
on
7:44:00 AM
Rating: