MAMA KANUMBA ATOA YA MOYONI KUHUSU MWANAE SOMA HAPA

MAMA wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amesema kama kuna msanii anataka kufikia ‘levo’ za mwanaye basi asali sana.
Mama wa aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Akifunguka mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, mama Kanumba alisema pengo la mwanaye katika sanaa linaonekana wazi hivyo ni vyema kwa anayetaka kuliziba kufuata nyayo zake.
”Miongoni mwa siri kubwa za mafanikio kwa mwanangu zilizomfanya awike kuliko wengine ni kupenda kuthubutu, kusali sana na kutokuwa na wivu wa maendeleo kwa kujiepusha na majungu.
Marehemu Steven Kanumba,enzi za uhai wake.
“Tatizo wasanii wetu hawa hawapendi kuthubutu wamekalia tu kufanyiana majungu, hawapendi kuona mwenzao anafanikiwa wanaanza kumfitini, ni vizuri wangejifunza kitu kwa Kanumba ambaye alipenda kuthubutu,” alisema mama Kanumba.
MAMA KANUMBA ATOA YA MOYONI KUHUSU MWANAE SOMA HAPA MAMA KANUMBA ATOA YA MOYONI KUHUSU MWANAE SOMA HAPA Reviewed by Unknown on 12:38:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.