POLISI mkoani Morogoro wanamshikilia Tausi Omary (30), mkazi wa kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kujeruhi mtoto wa dada yake, Jafari Mashaka (11) kwa kumchanachana mguuni kwa wembe na kisha kuweka chumvi kwenye vidonda, kwa madai ya kumwimbia fedha kiasi cha Sh 4,500.
Mashaka,
mwanafunzi wa Memkwa wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiwanja
cha Ndege, alikutwa na majanga hayo, majira ya saa 12 ya asubuhi ya
Novemba mosi mwaka huu, nyumbani kwao wanakoishi mtaa wa Kiwalani, kata
ya Chamwino.
Mtuhumiwa
huyo ambaye ni mama mdogo wa Jafari alitiwa nguvuni jana na Polisi
kufuatia wasamaria kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kiwalani, Salvatory Lipembe , ambaye naye alilifikisha suala hilo Kituo
Kikuu cha Polisi cha Morogoro.
Kukamatwa
kwa mwanamke huyo, kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Morogoro, Leonard Paulo, kupitia Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sophia
Ngasso, wa Dawati la kupambana na ukatili wa kijinsia na watoto la
Polisi Mkoa.
Kamanda
alisema baada ya kuwasilishwa kwa taarifa kituoni hapo na Mwenyekiti wa
Serikali za Mtaa, walikwenda kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya kuhojiwa
zaidi kuhusu jambo hilo.
Alisema
mama mdogo huyo alidai alifanya hivyo baada ya Jafari kuiba Sh 4,500 na
ndipo alipompiga kwa fimbo na hatimaye kumchana kwa wembe katika mguu
wake kwa sababu ya hasira.
Mtoto
huyo, akisimulia kisa hicho alidai kuwa kilimkuta majira ya saa 12
asubuhi ya Novemba 2, mwaka huu na kwamba alichuka fedha hizo Sh 4,500
baada ya kuzidiwa na njaa, na ndiyo mama yake mdogo alipogundua
alimkamata na kumpiga fimbo na baadaye kumchana na kiwembe mguuni, kicha
kumtia chumvi.
Alisema,
baada ya kukamilisha uchunguzi, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani
kwa mujibu wa sheria , ambapo pia alisisitiza suala la kuheshimika
msingi ya sheria na haki za binadamu wakiwemo watoto.
MASKINI MTOTO MDOGO ACHANWA NA VIWEMBE , VIDONDA VYAEKWA CHUMVI
Reviewed by Unknown
on
1:51:00 AM
Rating: