Mji
wa Morogoro umekumbwa na matukio mfululizo ya mafumanizi ambapo baada
ya ticha wa shule ya msingi kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa
kubondwa kwa kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa
upadri kufumaniwa, mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la
njemba mwenye asili ya Kiarabu limetokea.
Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed.
Kwenye Kata ya Mazimbu mjini hapa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja
la Hemed, anadaiwa kunaswa laivu na mke wa mtu kwenye chumba anachoishi
kilichopo Mtaa wa Boma mjini hapa.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua
Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo
hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo
likiwa bichi.
Wakinamama hao wakifanya juhudi kumtoa mke wa mtu (mwenye sidiria) eneo la tukio.
Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’ (umati), Hemed alidaiwa kuwa
amekuwa na tabia ya kuwarubuni na kumwaga fedha mbuzi kwa wake za watu
na kuserebuka nao ndani ya ‘geto’ lake jambo lililowafanya wenye wake
zao kumwekea mtego ambao ulipofyatuka ukamnasa majira ya saa 3:00
asubuhi.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo
alisema kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa
kwa jina moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Mashuhuda wa tukio hilo wakipiga chabo dirishani kwa mwarabu aliyenaswa.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwenye eneo la tukio, mume wa Husna
aliyejitambulisha kwa jina moja la Siri alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimuaga
mke wangu nakwenda Mwanza kwenye shughuli zangu za biashara. Nikiwa
Mwanza nilijulishwa na majirani kwamba mke wangu kila siku anaacha
watoto wetu kwa mama yake na kwenda kulala kwa Mwarabu.
Raia wenye Hasira kali wakiwa eneo la tukio.
“Ukweli kama mwanaume nilipatwa na hasira, nikatafuta ndege nikarudi hapa (Morogoro).
“Nimeelekezwa
kwa Mwarabu na jamaa waliokuwa wamemwekea mtego, nilipofika
nilichungulia dirishani, nikamuona mke wangu na Mwarabu wakiwa
kitandani.
“Nilihisi kupooza mwili na roho ilikuwa inaniuma sana.”
Mwarabu(mwenye koti jekundu) aliyenaswa na mke wa mtu akiwa chini ya ulinzi.
Aliongeza: “Mimi na mke wangu tumefunga ndoa ya Kiislamu, tuna watoto
wawili, mmoja ana umri wa miaka mitano na wa pili ana mwaka mmoja na
miezi saba.
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
Mtuhumiwa (mwarabu) akichukuliwa kwa mahojiano zaidi.
Kwa upande wake Husna ambaye alisitiriwa na wanawake wenzake waliokuwa
wakimficha, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alimjia juu mwanahabari
wetu na kumtolea maneno ya shombo.
Naye Mwarabu huyo alipohojiwa, pia alimtolea vitisho ‘kamanda’ wetu.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.
Baadaye viongozi wa Kata ya Mazimbu wakiongozwa na Afisa Mtendaji,
Brioht Sospeter na polisi mmoja walifika eneo la tukio wakawaondoa
wawili hao na kuwapeleka ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.