Kauli ya NBC kuhusu taarifa za KUWAIBIA fedha wateja kwenye ATM !



Uongozi wa NBC umebaini kuwepo kwa ujumbe kupitia mitandao ya jamii unayohusisha NBC na wizi wa fedha za wateja kwa kupita mashine za kutolea fedha (ATM). Ujumbe huo huo unahamasisha wateja kutoa fedha kwenye akaunti zao.


NBC tunapenda kuwafahamisha wateja wetu na umma kwa ujumla kwamba ujumbe huo hauna ukweli wowote. Papo hapo, matukio ya miamala ya wizi ni tatizo ambalo linaendelea kutafutiwa utatuzi na mabenki yote yaliyo chini ya Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).

Tunapenda kuwahakishia wateja wetu na umma kwamba NBC inaendelea kudhamiria kuwapatia wateja wetu huduma bora na ya kisasa.

Imetolewa na uongozi
Kauli ya NBC kuhusu taarifa za KUWAIBIA fedha wateja kwenye ATM ! Kauli ya NBC kuhusu taarifa za KUWAIBIA fedha wateja kwenye ATM ! Reviewed by Unknown on 11:57:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.