Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ akiwa na bebi wake Zuwena Mohammed ‘Shilole’.
Stori: Waandishi Wetu
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
JAMBO limezua jambo, saa chache baada ya mwanadada mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
Ads by InfoAd Options
Shilole alivalishwa pete hiyo katika
sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika ‘apartment’ za Baraka
Plaza, Mikocheni jijini Dar ambapo mara baada ya mwanadada huyo kukata
keki na kuwalisha watu mbalimbali waliohudhuria, ndipo Nuhu
alipomsapraizi mwanadada Shilole kwa kumvisha pete hiyo.
Kitendo hicho kilionekana kukubalika na
waalikwa wengi, lakini wengine hawakufurahishwa nacho kwa madai eti
kwamba Nuhu ni mdogo kuliko Shilole hivyo hakustahili kuvisha pete mtu
mwenye umri kama dada’ke.
“Mh! Mwenzangu hii kali, mimi siku zote
Nuhu niliamini hayupo serious kutembea na Shilole maana ni mkubwa kuliko
yeye lakini sasa hapa kanishangaza kweli, kwa nini asitafute mdogo
mwenzake?,” alisikika dada mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Hata hivyo licha ya masengenyo hayo
kusambaa chini kwa chini, Nuhu aliwakata watu vilimilimi kwa kutamka
hadharani kuwa wanapendana na Shilole hivyo haoni ajabu kama kuna watu
hawatakubaliana na penzi lao.
‘Shilole’ akiwa pembeni ya keki yake ya bethidei wakati wa sherehe yake ya kuzaliwa.
“Tukio linalotendeka hapa limepewa
baraka zote na wazazi wetu wameridhia mimi na mchumba wangu tuoane na
hii ni hatua ya kwanza tu mengine yatafuata na msishangae sana kuona
wazazi wetu hawapo eneo hili ni kwamba wanatambua kinachoendelea hapa.
Ads by InfoAd Options
“Najua wengi mtakuwa na maswali kuhusu
hili, mimi na yeye tunapendana na ndiyo maana leo hii namvisha pete
mpenzi wangu na Mungu atatujaalia katika maisha yetu,” alisema Nuhu na
sherehe ikaendelea kwa watu kula na kunywa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa
mbalimbali akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Wellu Sengo
‘Matilda’, Shettah, Martin Kadinda, Mh. Temba, Chegge, DJ Choka na DJ
Tass.
Steve Nyerere aliyekuwa MC wa shughuli
hiyo alisema Shilole ni shemeji yake kwani yeye ni kaka yake Nuhu, na
kwamba tukio linalofanyika hapo, wao kama ndugu wamekubaliana na ndoa
itafungwa.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.
PETE YA SHILOLE YAIBUA MAZITO!
Reviewed by Unknown
on
11:49:00 PM
Rating: