SAID FELLA ADAI ALIPIGWA MKWARA NA MASHEHE KWA KUMVALISHA SURUALI BIBI CHEKA!




Said Fella amedai kuwa mashehe waliwahi kumfuata na kumtaka aache tabia ya kumvalisha suruali Bibi Cheka.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi TV, Fella alisema mashehe hao walimfuata na kumwambia Bibi Cheka anatakiwa kuswali na sio kufanya muziki.

“Kuna muda si unajua dini yangu ya Kiislam wakatokea mashehe ‘ehh bwana unajua yule bibi mzee, kwanini mnamvalisha jeans!
"Na mimi naheshimu kila pande nikawaambia vizuri ‘lakini bibi huyu kuna mabibi wangapi wanaomba hela kwenye mtaa na mpaka serikali inakataza, kama huyu kaona nafuu yake kujipatia ugali kupitia huu mwaache nisafiri naye’ wakaniambia ‘bwana huyu bibi na geji yake anatakiwa kubeba msahafu’ lakini mimi bado naongea nao wale mashehe kwa sababu mwisho wa siku bibi anatakiwa asaidiwe, unakumbuka ametengeza nyimbo moja na Temba,” alisema Fella.
SAID FELLA ADAI ALIPIGWA MKWARA NA MASHEHE KWA KUMVALISHA SURUALI BIBI CHEKA! SAID FELLA ADAI ALIPIGWA MKWARA NA MASHEHE KWA KUMVALISHA SURUALI BIBI CHEKA! Reviewed by Unknown on 6:00:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.