Mapenzi
bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto
Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye
‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a
Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika
siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Akizungumza
katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge
jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma maneno baada ya
kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au Dangote
hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.
Alifunguka:
“Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa
kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu
pia.
“Siwezi
kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya
kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na
mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada
ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri
ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli
nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini
Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea,
watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado
nahitaji kujitangaza zaidi.”BOFYA KUONA SABABU HIZO>>>
DIAMOND PLATNUMZ AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA MPENZI WAKE MPYA ZARI!
Reviewed by Unknown
on
11:39:00 PM
Rating: