MZAZI MWENZIE WA MBUNGE SUGU AFUNGUKA MAZITO ALIYOPITIA 2014!



Mwigizaji wa filamu, Faiza Ally ambae ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Mh.Joseph Mbilinyi "Sugu" ameelezea ni kwajinsi gani mwakuu mabao yalivyo muendea vibaya ikiwemo kupeperuka kwa ndoa yao, lakini sasa anajipanga kuanza vyema mwakani.

Wakati huu mwaka unaanza, nakumbuka nilikua Mbeya mwezi January ilikua ni baada ya kumbatiza Sasha wakatti wa Christmas,wakati huo nilikua na matumaini makubwa sana pia tulikua tumepanga ndoa yetu iwe mwezi wa tano na ni kwa sababu ni siku ya kuzaliwa kwa mwenzangu!
Lakini January hiyo hiyo mambo yakibadilika vibaya sana pia nikarudi dar na kuanza maisha mapya ! Wakati narudi na mwanangu hata sikujua nianzie wapi nifanye nini! Lakini namshukuru M.Mungu nimeweza kufanya nilivyo fanya na Nipo nilipo sasa! sababu ya kuandika haya ni kwa sababu ya kuwajuza watoto wakike kuwa tunaweza tukiamua! Binafsi sikujua itakuaje Lkn niliamua na nimeweza japo haikua rahisi ... Nimelalamika sana ,nimelia na nimefurahi pia nimeshukuru na sehemu zingine nimeonekana Kama chizi au nimerukwa na akili Lkn yote ilikua ni kwa sababu ya uchungu nilio pata kwa kipindi chote ! Sasa mwaka huu unaisha nataka niyaache yote nyuma yalipita nianze na mwaka mpya na mambo mapya! Kwa hili namuomba Mungu aniwezeshe Insha Allah niweze ku songa na nirudi kuwa yule Faiza ninae mjua mimi Insha Allah

Pia nawaombea Mungu wenzangu wote walio pata matatizo kwa namna yoyote mungu awabariki wawe na mwanzo mzuri ktk mwaka ujayo na wale walio barikiwa mungu awape baraka zaidi na Insha Allah awaepushe kwa mabaya! Mimi na mwanangu Sasha tunawatakia heri na mafanikio ktk mwaka ujao Insha Allah ! Pia marafiki zangu wote naomba mjue kwa namna Fulani mnanifanya nijisikie furaha japo kuna wengine wanakera .... Amani iwe juu yenu ... Ameen –Faiza alimaliza
MZAZI MWENZIE WA MBUNGE SUGU AFUNGUKA MAZITO ALIYOPITIA 2014! MZAZI MWENZIE WA MBUNGE SUGU AFUNGUKA MAZITO ALIYOPITIA 2014! Reviewed by Unknown on 9:52:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.