
Akizungumza na Global TV Online kwenye ofisi za gazeti hili Bamaga-Mwenge jijini Dar, hivi karibuni, Diamond alifunguka: “Nilimpa (Penny) mimba ya kwanza, sikuamini ikabidi twende naye hospitalini tukapime, akaambiwa anayo…nikafurahi nikampiga na ndinga (gari) mpya siku hiyohiyo, nikamwambia mama tulia unizalie mwanangu.
“Sikukaa sana akaniletea maneno…oooh mara hivi mara vile…eti imetoka. Nikasema poa, labda haikuwa riziki. Nikampa ya pili, nayo pia akatoa. Nikasema bora niachane naye na huo ndiyo ukawa mwisho wa mimi na Penny.”
KILICHOFUATA
Baada ya habari hiyo kuchapishwa kwenye gazeti ndugu la hili, Amani wiki iliyopita, Penny alijibu mapigo na kudai kwamba ni kweli staa huyo alikuwa akimridhisha kimapenzi lakini hakuwa na uwezo wa kumpachika mimba kama alivyodai.“Diamond ni mwanaume kama wanaume wengine lakini hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba, muulizeni vizuri tatizo ni nini,” alisema Penny.
Alipofikishiwa taarifa hizo, Diamond hakutaka kufunguka kwa madai kwamba kuna vitu huwa hataki kuvisema kwa kuwa ni mtoto wa kiume na huwa anahifadhi siri nyingi za wanawake.DIAMOND ANA TATIZO?
Kwa mujibu wa Penny ni kwamba alikuwa akimridhisha vizuri kimapenzi hivyo hana tatizo la nguvu za kiume isipokuwa hawezi kumpa mwanamke kibendi.
KITAALAM ZAIDI
Akizungumzia tatizo la Diamond (kama maelezo ya Penny ni kweli), mtaalam wa masula ya tiba ya uzazi wa gazeti hili (jina tunalo) alisema kuwa mwanaume anaweza kumridhisha vizuri mwanamke wanapokuwa kitandani isipokuwa akashindwa kumpa ujauzito.
HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA DIAMOND PLATNUM..!! SOMA HAPA UJUE KILICHOTOKEA
Reviewed by Unknown
on
8:31:00 AM
Rating:
