Moja ya kivutio kikubwa kwa wakazi wa jiji la mwanza ambao walisherehekea Sikukuu ya Krimasi ilikuwa ni kupiga picha pamoja na samaki huyu.
Mamia ya wakazi wa jiji la mwanza wakipiga picha za kumbukumbu maeneo ya Samaki raund about ya katikati ya jiji la Mwanza.Maafisa wa usalama barabarani walikuwepo katikati ya Jiji kuhakikisha usalama unatawala jijini hapa kwa kuepusha ajali za hapa na pale.
Wakati wengine wakisherehekea sikukuu ya Krismasi Madreva daladala walikuwa wakikusanya pesa mtindo mmoja.
Wakazi wa jiji la mwanza wakijivinjari maeneo ya Kemondo jijini hapa.
Wakazi wa jiji la mwanza wakisherekea sikukuu ya Krismasi kwa kupiga picha, hapa walikuwa wakisubiri picha walizopigwa.
Katika kusherehekea siku kuu ya Krismasi wakazi wa jiji la Mwanza wengi wao starehe yao ilikuwa kupiga picha za kumbukumbu kutokana na mwaka 2014 kuelekea ukingoni huku baadhi yao wakitumia fursa hiyo kuzunguka maeneo mbalimbali jijini hapa lakini gumzo zaidi ilikuwa ni umati wa watu waliokuwa wamesimama nje kidogo ya eneo la kusafishia picha jambo ambalo lilileta uhalisia kwamba kweli leo ni siku ya Krismasi.
HIVI NDIVYO SIKUKUU YA X-MASS ILIVYO TIKISA JIJI LA MWANZA , JIONEE MWENYEWE
Reviewed by Unknown
on
8:00:00 AM
Rating: 5