BAADA YA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA, ROSE MUHANDO ANASWA AKITUMBUIZA NA KITUMBO!!

BAADA ya kudaiwa kulipwa fedha na kuingia mitini kwenye matamasha mbalimbali, mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani) amenaswa akitumbuiza jukwaani akiwa na ujauzito mkubwa. 

 
Mwanamuziki ‘grade one’ wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando akitumbuiza.

Tukio hilo lililowashangaza watu wengi lilitokea Jumapili iliyopita katika Kijiji cha Ilongero jimbo la Singida Kaskazini kulipokuwa na mkutano wa hadhara aliokuwa akiuhutubia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.

Wakati wananchi wakimsubiri Nyalandu ambaye pia ni mbunge wa Singida Kaskazini ahutubie, zilitangulia burudani za hapa na pale ndipo baadaye alipopanda Rose akiwa na kitumbo ‘ndii’ na kusababisha minong’ono chini kwa chini.

“Mh! Jamani huyu ni Rose kweli au macho yangu? Si angepumzika? Mbona tumbo tayari kubwa hivi, hata kama ni kusaka pesa lakini si kwa staili hii, kuna wakati mtu inabidi fedha uzipe kisogo,” alisikika mmoja wa wananchi.

Hata hivyo sambamba na watu kutilia shaka juu ya afya yake, Rose alionekana kulimudu vyema jukwaa kwa kutumbuiza nyimbo zake huku akiimba kwa staili ya kurukaruka kama kawaida.

Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa Ilongero na jimbo zima la Singida Kaskazini, mbali na kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, Nyalandu alitangaza nia ya kugombea urais mwakani.
BAADA YA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA, ROSE MUHANDO ANASWA AKITUMBUIZA NA KITUMBO!! BAADA YA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA, ROSE MUHANDO ANASWA AKITUMBUIZA NA KITUMBO!! Reviewed by Unknown on 10:46:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.