MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA AIDRIS AMFUNGUKIA LULU MICHAEL WA BONGO MOVIE

KWA mara ya kwanza baada ya kutua Bongo, Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshort (2014), Idris Sultan amemfungukia mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kudai ni rafiki yake wa karibu.
Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Sultan.
Kabla mshindi huyo hajakanyaga Bongo, Lulu alishambuliwa mitandaoni baada ya kujinadi kuwa na urafiki wa karibu na Idris lakini kwa kauli hiyo,
imeonesha dhahiri wawili hao ni marafiki wa kweli tofauti na mitazamo ya wadau mitandaoni.
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Lulu ni rafiki yangu wa muda mrefu, hakuna kingine zaidi ya urafiki. Tutaendelea kuwa marafiki hata baada ya ushindi huu,” alisema Idris, juzi alipokuwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam (The Kilimanjaro).
MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA AIDRIS AMFUNGUKIA LULU MICHAEL WA BONGO MOVIE MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA AIDRIS AMFUNGUKIA LULU MICHAEL WA BONGO MOVIE Reviewed by Unknown on 1:25:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.