MSANII TOKA NIGERIA DAVIDO AONYESHA CHUKI ZA WAZI WAZI BAADA YA IDRIS KUJIBEBEA MIL 500 ZA BBA


Msanii Davido 

Hii ndio tweet ya Davido Muda mfupi tu mara baada ya Idris Kutangazwa Mshindi wa BIG BROTHER AFRICA HOTSHOS 2014.

Na Josephat Lukaza - Wa Lukaza Blog
Mara tu baada ya Idris Sultani Kutangazwa mshindi wa Big Brother Africa hotshots 2014 hatimaye Msanii kutoka nchini Nigeria Davido aonyesha chuki binafsi kwa Watanzania na Tanzania kwa Ujumla mara baada ya kutweet "They Cheat Again lol" katika ukurasa wake wa tweeter.

Hii inaonyesha wazi kuwa Davido amechukia, na kuumia sana kiasi kwamba akaamua kuonyesha waziwazi chuki zake binafsi kwa kutweet "They Cheat Again lol" Hii inaonyesha wazi kuwa Davido anawachukia sana watanzania na Tanzania kwa ujumla kutokana na Kugalagazwa na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Tanzania Diamond Platnum katika Tuzo za Muziki za Channel O zilizofanyika huko huko Afrika Kusini 


Tweet hii imekuja mara tu baada ya Mshiriki Kutoka Nchini Tanzania Idris Sultan kutangazwa Mshindi wa SHindano la Big Brother Africa Hotshots 2014.

Ikumbukwe kuwa Msanii Davido akuweza kuondoka hata na Tuzo moja katika Mashindano hayo ya Channel O yaliyofanyika hivi karibuni Nchini Afrika Kusini

Tweet hiyo imeonyesha wazi kabisa Davido anachuki binafsi kwa Watanzania na Tanzania mara baada ya kugalagazwa na Staa wa Nyimbo ya nitampata wapi Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania.
MSANII TOKA NIGERIA DAVIDO AONYESHA CHUKI ZA WAZI WAZI BAADA YA IDRIS KUJIBEBEA MIL 500 ZA BBA MSANII TOKA NIGERIA DAVIDO AONYESHA CHUKI ZA WAZI WAZI BAADA YA IDRIS KUJIBEBEA MIL 500 ZA BBA Reviewed by Unknown on 11:00:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.