Basi
liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa
likitokea Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.
Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia.
Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa
magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa
mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata
hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria
wote wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo.
Haikupita muda mrefu baada ya abiria
kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha
kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika
ajali hiyo.
GARI LAINGIA MTARONI LIKIPANDA MLIMA KITONGA
Reviewed by Unknown
on
12:42:00 AM
Rating: