DIAMOND PLATNUMZ NA WEMA SEPETU KURUDIANA TENA NA KUFUNGA NDOA RASMI

UNAJIMU! Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Shehe Yahya amesema kuwa, penzi la mastaa wa Kibongo,Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ bado halijafika mwisho, watarudiana na kufunga ndoa.
Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumzia penzi la wawili hao ambao siku chache zilizopita wameripotiwa kumwagana alisema, hali hiyo ni ya mpito tu haimaanishi kuwa hiyo ndiyo tamati ya
mapenzi yao, sababu nyota zao zinategemeana japo ya Wema ina nguvu kubwa kuibeba ya Diamond.
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu.
“Msifikiri kwamba penzi lao ndiyo limefika mwisho, hakuna kitu kama hicho ni mara ngapi wameachana na kurudiana hata hili la sasa natabiri watarudiana,” alisema Malim.
DIAMOND PLATNUMZ NA WEMA SEPETU KURUDIANA TENA NA KUFUNGA NDOA RASMI DIAMOND PLATNUMZ NA WEMA SEPETU KURUDIANA TENA NA KUFUNGA NDOA RASMI Reviewed by Unknown on 11:14:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.