SERIKALI ya Tanzania imekataa rasmi
kutambua ndoa za jinsia moja (ushoga) kama moja ya agenda za maendeleo
katika malengo ya milenia 2015 mpaka 2030 katika mkutano wa Umoja wa
Mataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye
mkutano wa majadiliano ya malengo ya milenia yanayotazamiwa kumalizika
mwakani na kuanza malengo mapya, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Celestine Mushy amesema serikali ya Tanzania imekataa
kutambua ushoga kama moja ya agenda za maendeleo.
“tunatambua haki za binadamu, usawa wa
kijinsia kati ya wanaume na wanawake na hata katiba yetu pendekezwa
imetoa haki za sawa kati ya wanaume na wanawake lakini katika swala la
kutambua ndoa za jinsia moja hilo tumekataa,” amesema Balozi Mushy
Amesema kwamba tumewaambia nchi
zilizoendelea na wahisani wa maendeleo katika Umoja wa Mataifa kwamba
swala la ndoa za jinsia moja (ushoga) si agenda ya watanzania na si
agenda ya maendeleo.
Balozi Mushy aliongeza kwamba serikali
ya Tanzania imeweka msimamo huo zaidi hivi karibuni na Rais Jakaya
Kikwete aliagiza hivyo kwa maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na
Waziri husika kukataa shinikizo la kukubali swala ushoga kama agenda za
maendeleo.
Amesema kwamba watanzania wanataka
maswala yanayowagusa kama vile maji, elimu, huduma bora za afya,
miundombinu ya umeme, ajira, umaskini na kuondoa umaskini wa kipato.
Balozi Mushy alifafanua zaidi kwamba
mambo ya ushoga na ndoa za jinsia yanakwenda kinyume na maadili ya
watanzania, maisha, historia, utamaduni, mila na desturi za mtanzania
sinakataza maswala ya ushoga.
Amesema kwamba serikali inatambua kwamba
sheria ya mwenendo wa makosa ya kujamiiana yaliwekwa na mkoloni
mwingereza kabla ya uhuru na serikali ya Tanganyika imerithi kutoka
kwenye serikali ya mwingereza.
Tanzania Yakataa Rasmi Mambo ya Ndoa za Mashoga na Wasagaji 'Ndoa za Jinsia Moja'
Reviewed by Unknown
on
11:33:00 PM
Rating: