AIBU:MWESHIMIWA MBOEWE AFANYA MAMBO YA AIBU MBELE YA WATOTO ALA DENDA NA MKE WAKE UKU AKIPIGWA PICHA
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani (Bungeni), Freeman Mbowe, wiki iliyopita
alipamba vilivyo mitandao ya kijamii, haikuwa kwa sababu ya tishio la
maandamano kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wala Katiba Mpya,
‘topiki’ ilikaa kimapenzi zaidi.
Watu aah! Mheshimiwa Mbowe, ooh hivi, mara vile! Tathmini ya gazeti hili
inaonesha kuwa asilimia kubwa wanampongeza mbunge huyo wa Hai
(Chadema), kwamba ni mume mzuri na baba bora wa familia yake.
Hujanyaka topiki? Wiki iliyopita katika mitandao zilienea picha za Mbowe
akiwa kwenye sherehe ya kifamilia, iliyofanyika Oktoba 12, mwaka huu
kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Serena Hotel, Dar es Salaam, huku
zikimuonesha anambusu mkewe, Dk. Lillian Mbowe kwa hisia kali za
malovee.
KWA NINI PONGEZI?
Uchunguzi wa gazeti hili katika mitandao ya kijamii kupitia ‘komenti’ mbalimbali pamoja na maoni ya watu kadhaa waliohojiwa mitaani na mwandishi wetu, picha hizo zinampambanua Mbowe kama kiongozi wa kisasa ambaye anajua jinsi ya kuwajibika kifamilia.

Watoa maoni wengi, wamemfananisha Mbowe na Rais wa Marekani, Barack
Obama kwamba ni mfano wa kuigwa katika viongozi wanaojali familia.“Obama
kwa mkewe Michelle na wanaye Sasha na Malia, ni wazi yeye ni baba bora
wa familia. Kamanda Mbowe amedhihirisha kuwa siasa hazimuweki mbali
mpaka akasahau familia, nimependa sana picha hizi za Mbowe na familia
yake,” alisema Julie Macklin wa Sinza, Dar es Salaam.Mh. Freeman Mbowe akishoo love kwa mkewe.
Pingu Mabula katika ukurasa wake wa Facebook, aliandika: “Nimefurahishwa
sana na hii picha (inayomuonesha akimkisi mkewe, huku watoto wao watatu
wakiwa wanawatazama kwa tabasamu), natamani viongozi wote wawe na
mahaba ya kuridhisha kwa familia zao kama hivi.”
Mwanahawa Red-guard, aliweka picha kama ambayo Pingu aliitundika
Facebook kisha akasindikiza kwa maneno: “Njia ya muongo ni fupi sana,
kuna waliokuwa wanadai kamanda Mbowe na mkewe hawaelewani, mara picha
haziendi, hii ni kuonesha jinsi ambavyo mtu mzima alivyotulia na mkewe.
“Unakuwa na mkeo lakini hutaki kumuonesha upendo, watoto hawaoni upendo
wa wazazi wao mpaka nao wanaathirika kisaikolojia, lakini picha hii ni
wazi Mbowe anajenga kitu upendo ndani ya familia, wazazi wanapendana,
watoto pia watapendana tu, vilevile wakiwa na familia zao watazijenga
kwa upendo pia.”
PICHA PENDWA
Pamoja na ukweli kwamba picha za Mbowe akimbusu mkewe ni nyingi lakini moja iliyovutia wengi ni ile ambayo mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anambusu mkewe, huku watoto wao ‘firstborn’ Dudley, Nicole na Denis wakiwatazama kwa tabasamu.

Mh. Freeman Mbowe akimbusu mkewe huku watoto wakitabasamu
Uchunguzi umeonesha kuwa picha hiyo ndiyo iliyoongoza kwa ‘kupostiwa’
katika Mitandao ya Kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram na mingine,
huku blogu kadhaa zikiifanya habari, vilevile ikitumwa sana katika
makundi ya WhatsApp.
MCHUNGAJI HARRIS KAPIGA APONGEZA
Mchungaji wa Kanisa la Nchi ya Ahadi ambaye pia ni mhamasishaji wa masuala ya kiuchumi na familia, Harris Kapiga, aliipongeza picha hiyo na akasema hashangai kwa nini inapendwa sana na watu kutokana na ujumbe inaofikisha.

Kapiga alisema: “Ni picha bora sana kwa familia. Ipo hivi, wewe baba
ukitaka uwape zawadi bora kabisa watoto wako basi mpende mama yao. Ndiyo
maana katika picha hiyo watoto wanatabasamu, ni zawadi kubwa sana
ambayo Mbowe amewapa kwa kuonesha jinsi anavyompenda mama yao.
“Kingine ni kwamba mwanaume amepewa mamlaka, inapotokea mume anambusu
mkewe hadharani kama Mbowe alivyofanya, inaonesha jinsi ambavyo upendo
wake kwa mkewe hauna shaka. Ni upendo wa dhati kabisa.
“Tafiti zinaonesha pia kuwa familia nyingi za wanasiasa huchukia siasa
kwa sababu ya kukosa uwepo wa baba kwa muda mwingi. Vivyo hivyo kwa
madaktari, wachungaji na kadhalika, huchukia huduma za baba zao lakini
Mbowe ameonesha kuwa kiongozi mkubwa wa kisiasa hakuzuii kuwajibika
ipasavyo ndani ya familia.”
MWANASAIKOLOJIA CHRIS MAUKI ANENA
Mtaalamu wa Saikolojia na Uhusiano ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Chris Mauki, alisema kuwa picha za Mbowe akimbusu mkewe hadharani zimemuongezea thamani kijamii kwa sababu watu wanawapenda wanaume wanaobeba majukumu ya kifamilia.

“Unadhani kwa nini Obama ni kiongozi mashuhuri sana duniani na anapendwa
sana na watu, ni kwa sababu ya ile tabia yake ya kuwa karibu na familia
yake. Kuna watu wanampenda Obama si kwa sababu ya nguvu kubwa aliyonayo
kisiasa, ni kwa sababu anajipambanua kuwa baba bora wa familia.
“Jamii kubwa sasa inakosa upendo wa wazi kutoka kwa akina baba. Akina
baba wengi wanaona kumbusu mkewe hadharani na kuwa karibu na familia
siyo suala lenye maana kubwa, kwa hiyo wale ambao wanayafanya hayo
waziwazi huonekana mashujaa.
“Mbowe anapongezwa kwa sababu ni shujaa kwenye jamii kwa sababu
alichokifanya wengi hawakifanyi. Familia nyingi zinakosa upendo na
kufanya mpaka watoto kuathirika kisaokolojia, watoto wanaharibika,”
alisema Dk. Mauki na kuendelea:
“Viongozi wa kisiasa wanapokuwa wanajali familia zao, inatia hamasa
kubwa. Hata kama nyumbani hawajibiki vizuri kifamilia lakini kwenye
jamii anapokuwa muwajibikaji na watu wanamuona, huvutia wengi na
kupendwa sana.”
KAMANDA MBOWE AFAFANUA
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema kuwa picha hizo zilipigwa siku ambayo kwa hakika alikuwa mwenye furaha sana kutokana na mambo mawili yaliyogusa familia yake.

“Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza umri wa miaka 50 ya kuzaliwa,
vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa amemaliza shahada yake ya kwanza
Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa mambo hayo mawili, tuliona ipo
haja ya kufanya sherehe, ukizingatia watoto wetu wengine wawili Nicole
na Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi.
“Siku hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani
Azania Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel
kwenye Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa
kimeandaliwa, tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.
“Haikuwa sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa
sherehe ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu,” alisema
Mbowe.
AIBU:MWESHIMIWA MBOEWE AFANYA MAMBO YA AIBU MBELE YA WATOTO ALA DENDA NA MKE WAKE UKU AKIPIGWA PICHA
Reviewed by Unknown
on
12:55:00 AM
Rating: