Tumekuwa
tukipata taarifa zinazohusu matukio ya mauaji ambayo yamekuwa
yakijitokeza mara kwa mara nchini Tanzania, hali ambayo imeonekana
kukithiri katika siku za usoni huku jeshi la polisi likitoa ahadi ya
kufanya jitihada za kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wa matukio
hayo.
Taarifa iliyonifikia hivi punde kupitia Radio One Breaking News inahusu
kuuawa kwa mtuhumiwa namba moja wa kesi ya ulipuaji mabomu jijini
Arusha, Yahaya Hassan Omar kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la
polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.
Akitoa taarifa za kifo cha mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi wa mkoa wa arusha Lebaratus Sabas amesema marehemu yahaya hassan omari hela maarufu kwa jina la (sensei) ambaye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo alikamatwa wiki mbili zilizopita mkoani morogroro na kupelekwa arusha na bado alikuwa anaendelea kuhojiwa.
Kwa mujibu wa kamandaa sabas mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa marehemu yahaya, alikiri kuwa yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa matukio yote ya milipuko ya mabomu na ya kumwagia viongozi wa dini tindikali yaliyowahi kutokea mkoani arusha na maeneo mengine.

Aidha kamanda Sabas Amefaanua kuwa baada ya marehemu ambaye ni mtuhumiwa kukiri tuhuma hizo alikuwa bado anaendelea kutoa ushirikiano kwa kuanza kuonyesha vitendea kazi yakiwemo mabomu ambayo alidaiwa kuyaficha kondoa mkoani Dodoma.
Amesema wakati anasafirishwa walipofika eneo la kisongo katika barabara kuu inayoenda dodoma majira ya usiku alifanya jaribio la kutaka kutoroka na ndipo akapigwa risasi iliyomjeruhi mguu na kiuno na akafariki wakati anapelekwa hosipitali.
BREAKING NEWSSSSS: POLISI WAUA MLIPUAJI WA MABOMU ARUSHA AKIWA MBIONI KUWATOROKA
Reviewed by Unknown
on
8:22:00 AM
Rating: