NI aibu iliyoje! Mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, amekutwa ndani ya danguro moja lililopo Sinza ya Mapambano jijini Dar ikiwa ni mazingira ya kutatanisha.
OFM ambao walikuwa wameandamana na walinzi shirikishi ili kudhibiti usalama, walisimama kidete kutekeleza majukumu yao huku mwanaume huyo akitoa vitisho, kwamba atawaua kwa bastola waandishi, endapo hawataacha kupiga picha. Wakati akitoa vitisho hivyo alikuwa akielekea kwenye gari lake ambako alichukua kitu kinachofanana na chuma, kilichowafanya walinzi shirikishi kutimua mbio kuhofia kuuawa.
Wakiwa wamebaki peke yao, waandishi wetu walianza kupigwa na wasichana, mwanaume huyo na walinzi waliokuwa na fimbo, mawe na silaha nyingine za jadi. Baadaye mapaparazi wetu walifanikiwa kupiga simu kwa kamanda mkuu wa OFM ambaye naye aliwasiliana na polisi waliofika eneo hilo dakika chache mbele.
Pamoja na ujio wa polisi hao, mwanaume huyo ambaye wakati huo alikuwa ameshawasababishia majeraha waandishi wetu, aliendelea kuwa mbishi, hadi baadaye alipokubali kuingia kwenye gari lake na askari kuelekea Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akiwa njiani, mwanaume huyo aliliendesha gari kwa kasi na kutaka kuligongesha kwenye mti hali iliyomfanya askari aliyekaa mbele upande wa abiria na bunduki kuruka ili kunusuru maisha yake.
Askari mwingine aliyebaki ndani ya gari na waandishi alifanikiwa kumtuliza mtu huyo ambaye baadaye alipigwa pingu na askari kuendesha gari hadi kituoni. Ili kujua nini kiliendelea, fuatilia kesho kwenye Gazeti la Ijumaa maana jamaa huyo alilala kituoni hapo tangu Ijumaa usiku hadi Jumatatu iliyopita kutokana na hali ya mwandishi mmoja kuwa mbaya.
Ishu hiyo ilijiri usiku wa manane wa Ijumaa kuelekea Jumamosi ya wiki iliyopita. Awali, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global
Publishers ilipokea taarifa kutoka kwa vyanzo vyake kuwa ndani ya
danguro hilo, ameingia mwanaume huyo aliyeonekana kuwa na heshima zake
na kwa vile inaeleweka vitu vinavyoendelea, vyanzo vilikuwa na wasiwasi
naye!Bila kupoteza muda, kikosi kazi cha OFM kilifuatilia eneo hilo na
kufanikiwa kuingia ndani ya danguro hilo ambako walimkuta jamaa huyo
akiwa anazungumza na wasichana watatu ingawa haikueleweka mara moja
walikuwa wakizungumzia nini.
Baada ya kuwaona makamanda wa OFM, waliacha mazungumzo yao na
kuwatumbulia, lakini walipoanza kupigwa picha, ukaibuka mzozo mpya baina
ya watu hao wakisaidiwa na walinzi wanaolinda danguro hilo, dhidi ya
waandishi.OFM ambao walikuwa wameandamana na walinzi shirikishi ili kudhibiti usalama, walisimama kidete kutekeleza majukumu yao huku mwanaume huyo akitoa vitisho, kwamba atawaua kwa bastola waandishi, endapo hawataacha kupiga picha. Wakati akitoa vitisho hivyo alikuwa akielekea kwenye gari lake ambako alichukua kitu kinachofanana na chuma, kilichowafanya walinzi shirikishi kutimua mbio kuhofia kuuawa.
Wakiwa wamebaki peke yao, waandishi wetu walianza kupigwa na wasichana, mwanaume huyo na walinzi waliokuwa na fimbo, mawe na silaha nyingine za jadi. Baadaye mapaparazi wetu walifanikiwa kupiga simu kwa kamanda mkuu wa OFM ambaye naye aliwasiliana na polisi waliofika eneo hilo dakika chache mbele.
Pamoja na ujio wa polisi hao, mwanaume huyo ambaye wakati huo alikuwa ameshawasababishia majeraha waandishi wetu, aliendelea kuwa mbishi, hadi baadaye alipokubali kuingia kwenye gari lake na askari kuelekea Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Akiwa njiani, mwanaume huyo aliliendesha gari kwa kasi na kutaka kuligongesha kwenye mti hali iliyomfanya askari aliyekaa mbele upande wa abiria na bunduki kuruka ili kunusuru maisha yake.
Askari mwingine aliyebaki ndani ya gari na waandishi alifanikiwa kumtuliza mtu huyo ambaye baadaye alipigwa pingu na askari kuendesha gari hadi kituoni. Ili kujua nini kiliendelea, fuatilia kesho kwenye Gazeti la Ijumaa maana jamaa huyo alilala kituoni hapo tangu Ijumaa usiku hadi Jumatatu iliyopita kutokana na hali ya mwandishi mmoja kuwa mbaya.
AIBU GANI HII ! MUME WA MTU ANASWA NDANI YA DANGURO NA WAANDISHI WETU
Reviewed by Unknown
on
11:30:00 PM
Rating: