JESHI
la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kumkamata Michael William maarufu
(Michael dada), mkazi wa Kiluvya, wilayani Kisarawe anayetuhumiwa
kuhusika na matukio ya ubakaji wa vikongwe mkoani hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei
alisema jeshi hilo lilikuwa likimsaka mtuhumiwa huyo kwa kipindi kirefu
kutokana na kudaiwa kutenda makosa mbalimbali ya ubakaji wa vikongwe na
wanawake na kutokomea kusikojulikana.
Alisema,
William alitiwa mbaroni juzi baada ya kudaiwa kuhusika katika tukio la
wizi wa mifugo lililotokea wiki mbili zilizopita huko Kiluvya.
Pia
kamanda Matei alisema, mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika katika matukio
ya ubakaji zaidi ya 10 ambapo kabla ya kufanya vitendo hivyo alikuwa
akiwatishia wahusika kwa mapanga.
“Huyu kijana anayejiita Michael dada ni
maarufu kwa matukio ya ubakaji na alilisumbua jeshi letu mara kadhaa kwa
kunasua mitego aliyowekewa leo tumelazimika kumleta mbele yenu
waandishi ili mumuone ni mdogo lakini ametusumbua sana,” alisema.
William alikiri mbele ya waandishi wa
habari kuwa miaka ya hivi karibuni aliwahi kufanya unyang’anyi wa
kutumia silaha kosa ambalo lilimsababishia kuhukumiwa miaka 30 jela
Matei alisema kabla kifungo hicho
hakijamalizika mwaka 2011 na 2012, William alikata rufaa na kutolewa ili
kuendelea na taratibu nyingine na tangu hapo hakuonekana hadi polisi
walipofanikiwa kumkamata kwa kosa la wizi wa mifugo.
Hata hivyo William alikana kuhusika na
tuhuma zinazomkabili na kudai yeye sio Michael dada kama anavyoitwa bali
ni Michael William na tuhuma za ubakaji ni za kusingiziwa.
JAMAA ALIYEKUWA AKIWABAKA VIKONGWE ATIWA MBARONI HUKO KISARAWE PWANI
Reviewed by Unknown
on
2:38:00 PM
Rating: