HIZI NDIZO SABABU ZILIZOFANYA DIAMOND AZOMEWE


Written by @bikira_wa_kisukuma
DIAMOND ANA MAKOSA 3 MAKUBWA ALIYOTUTENDEA WATANZANIA:

1.Kosa la kwanza ni KUWA NA BIDII KWENYE MUZIKI WAKE...Hili ni kosa kubwa sana kwa Watanzania..Hakupaswa kuwa na bidii hivi..Angekuwa tu wa KAWAIDA kama wenzake waliopita ili AFULIE awaachie na wengine waje kwenye chati arudi Tandale kuuza Wali..

2.Kosa la 2 ni KUJITAMBUA YEYE NI NANI..Kwanini ajitambue wakati wenzie wenye majina walishindwa??Kwani yeye nani awe tofauti??Hii ni DHARAU KUBWA sana kwa Watanzania na Wanamuziki wenzie na inaonyesha ana KIBURI..Diamond kujua yeye ni Mwanamuziki mahiri na kutumia VALUE yake aliyoipata kwa mbinde kuiletea sifa Tanzania nje ya Mipaka ni KOSA KUBWA!

3.Kosa lake la 3 ni KUUHESHIMU MNO MUZIKI UNAOMPA HELA...Kwanini asiwe kama wakina Mr nanihii tu,kwani wao hawakuhit kama yeye?Mbona waliishi kawaida tu na kuuchukulia muziki poa hadi walipofulia na leo hata wakiingia Masai Club nobody cares..Kwani kufulia kitu gani?Diamond hakupaswa kuuheshimu Muziki kama kazi..Angefanya bora liende tu aimbe imbe yaishe..Sasa kujifanya Anatoa Collabo mara Davido mara Mafikizolo mara Trey Songs na K'Cee na Yemi Alade AMETUMWA NA NANI??Huku ni kutafuta sifa tu alipaswa awe mdogo milele awaachie na wenzie..
Kwa makosa haya ma3 WATANZANIA wameamua kumuadhibu..Diamond Anaringa...Ana dharau sana..Anaupenda sana Muziki uliompa JINA..HESHIMA..PESA..na ametafutiwa REPLACEMENT kwa sababu tu ANAHESHIMU MUZIKI KAMA KAZI na sio JUST SINGING FOR FAME...Watanzania tumeamua kuadhibu MTU ANAYEHESHIMU KAZI YAKE iliyomtoa from Zero to Hero na tutamshusha kwa lazima taji apewe mwingine..Watanzania tunataka Diamond awe another Mr Nice ili tupate kitu cha KUCOMPARE...Shida yetu kuu wala sio dharau ila ni KWANINI DAI HASHUKI????
Hardwork Pays!
Respect Pays!
Knowing Your Value Pays!
Kama alimpandisha MUNGU...Hakuna wa kumtoa pale...
Nasibu..wakomeshe..Toa ule wimbo na MAFIKIZOLO wiki ijayo tuone kama watazomea Spika za redio zao...
Nalala zangu MDOGO MDOGO...
HIZI NDIZO SABABU ZILIZOFANYA DIAMOND AZOMEWE HIZI NDIZO SABABU ZILIZOFANYA DIAMOND AZOMEWE Reviewed by Unknown on 1:37:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.