HILI NDILO DARAJA KUBWA LA KUTOKA ZANZIBAR HADI DAR ES SALAAM




Picha Ya Mfano wa Daraja Hilo Litakavyokuwa
Unaweza ukadhani ni ndoto lakini hii ni habari ya kweli baada ya Hifadhi ya jamii NSSF kutangaza uwezekano wa kujengwa daraja la kihistoria zaidilitakalounganisha Dar es salaam na Zanzibar.

Uwepo wa daraja hilo unaweza kuwa ni neema kwa Watanzania wote na hata nchi za jirani kwani itarahisisha shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa asilimia kubwa kwa kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.

Gazeti la HabariLEO liliripoti kuwa kwa sasa Shirika hilo lipo katika mazungumzo na wataalamu mbalimbali ili kuangalia uwezekano wa kujenga daraja hilo katika bandari ya Dar kwa upande wa Bara na Unguja kwa upande wa Visiwani.


Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ramadhan Dau alisema ujenzi wa daraja hilo si ndoto bali ni ukweli na tayari wameanza mazungumzo ya awali ili kutimiza malengo yao.

Umbali kati ya Dar na Zanzibar ni kilometa73.43 sawa na maili45.62 hivyo kuwepo na mradi huo ni jambo linalowezekana kwani kuna madaraja marefu zaidi duniani yanayounganisha upande mmoja wa bahari na mwingine.

Kwa sasa daraja refu zaidi duniani kote ni lile la Danyang-Kushan lililopo nchini China ambalo lina umbali wa kilometa 165 sawa na maili102.4 ambalo lilifunguliwa Juni mwaka 2011.
HILI NDILO DARAJA KUBWA LA KUTOKA ZANZIBAR HADI DAR ES SALAAM HILI NDILO DARAJA KUBWA LA KUTOKA ZANZIBAR HADI DAR ES SALAAM Reviewed by Unknown on 8:13:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.