Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo


Binafsi nimekuwa nikifuatilia hili suala la Diamond kuwa na msuguano na Davido tokea ushindi wa Idris Big Brother na nikiri kuwa Diamond hakupaswa kusema aliyosema dhidi ya Davido kwa sake ya urafiki wao!

Kwanini nasema hivyo? coz thamani ya urafiki waliokuwa nayo haiwezi kupotezwa kirahisi hivyo ingawa kuna watu wanafurahia tena kwa sababu za kitoto, kwa wale walioishasoma novel ya godfather nadhani wananielewa ninapozungumzia thamani ya urafiki! Kwani urafiki ni kama kula tunda na ukimaliza kuipanda mbegu yake ili siku utakapohitaji tena tunda uwe na sehem pa kulipata.

Sasa ninachoona ni giza kubwa mbele yetu sie mashabiki wa Diamond hatuoni ukweli tumejikinga kwenye kivuli cha uzalendo, hatutaki kukubali kuwa Davido kasaidia kupush mafanikio ya Diamond kwa kiasi fulani, mara baada ya number one rmx kutoka milango ilianza kufunguka kwa kasi kwa Diamond na hili wengi hatulioni bado tumefunikwa na kivuli cha uzalendo hatusimami kwny fact! ukitaka kuamini hili nenda youtube kaangalie number one rmx imeangaliwa na watu wangapi dhidi ya original version!

Kwa taarifa yako kuna gape la watu zaidi ya million mbili. Ndyo tunakubal Davido siyo mungu so Diamond hana haja ya kumtetemekea lakini kwa hili alipaswa kuonyesha heshima angalau kidogo kwani alichofanya ni ukosefu wa fadhila wa hali ya juu. mwisho na suggest Diamond afanye mpango amalize hili suala hata kama ni kimya kimya ili kuondoa tension iliyopo sasa.
Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo Tunapoficha makosa ya Diamond kwa kisingizio cha uzalendo Reviewed by Unknown on 11:16:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.