Kocha wa Pacquiao Anahofia Mayweather Ataingia Mitini May 2 (Picha)

Kocha wa Manny Pacquiao ana wasiwasi kuwa Floyd Mayweather anaweza asitokee kwenye pambano la kesho kutwa jijini Las Vegas.

Floyd Mayweather na Manny Pacquiao walikutana jana mbele ya waandishi wa habari jijini Las Vegas
Pacquiao na Mayweather wanakutana Jumamosi hii kwenye pambano lenye gharama kubwa katika historia ya ndondi duniani. Freddie Roach, kocha wa Pac alisema: Nina wasiwasi kama (Mayweather) atakuja usiku huo.

Mshindi wa pambano hilo atakabidhiwa mkanda huu wa thamani kubwa
“Sidhani kama mabondia wote wanahofia, ila sidhani kama alitaka kupigana. Alilazimishwa kupigana pambano ambalo hakulitaka,” aliongeza.

“Sijui tu kwanini Floyd amekuwa mkimya kwenye pambano hili. Maneno yake yana woga!

Hata hivyo Mayweather hakushangazwa na kauli ya Roach na kudai: Nitakuwepo. Niliongea uchafu siku za nyuma lakini pambano hili linajiuza lenyewe, hivyo sina haja.”
Kocha wa Pacquiao Anahofia Mayweather Ataingia Mitini May 2 (Picha) Kocha wa Pacquiao Anahofia Mayweather Ataingia Mitini May 2 (Picha) Reviewed by Unknown on 1:02:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.