LIST ya Mastaa wa BONGO Wanaongoza Kwa Kushusha Matusi Mtandaoni

Imekuwa ikielezwa kuwa wasanii ni kioo cha jamii. Kwa maana hiyo wanatakiwa kufanya mambo ambayo yanaweza kuigwa na wale wanaowatazama. Hata hivyo, maisha wanayoishi baadhi ya wasanii hayaakisi msemo huo.

Wengi wamekuwa wakikumbwa na skendo mbalimbali zinazowafanya wasiwe na vigezo vya kuitwa kioo cha jamii.

Miongoni mwa mambo yanayowafanya wakati mwingine wadharaulike ni kutoa maneno machafu, ‘live’ au kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Katika makala haya nitawazungumzia mastaa wanaoongoza kwa kutukana mitandaoni

Wastara Juma
Huyu Wastara amekuwa akiheshimika kwenye jamii kwa muda mrefu na alikuwa ni miongoni mwa mastaa wa kike ambao wangesimama na kuamua jambo wangesikilizwa kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka na kuwaaminisha watu.

Lakini katika siku za hivi karibuni alichafuka kwa kuingia katika orodha ya mastaa wanaotukana mtandaoni baada ya kumvaa mmoja wa mashabiki wake aliyemsemea mbovu na kumtukana matusi mazito


“Iweje anakubali kushushwa na mtu mmoja ambaye alikaa na kuamua kumvuruga, anasahau kama kuna kundi la watu linamheshimu?” Aliandika mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram baada ya kuona matusi hayo.

Amanda Posh

Wafuatiliaji wa mambo na hasa wale ambao wapo Facebook watakumbuka jinsi staa huyu wa filamu alivyomshambulia jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Joel.

Haikuwa ustaarabu kabisa kwa staa huyo kufanya hivyo kwani jambo lililomkasirisha angeweza kulipuuza na angebaki na heshima yake huku yule aliyemtukana akionekana mjinga.

Lakini ukiacha hilo, Amanda amekuwa akisifika kwa kutoa maneno machafu pale anapochokozwa, tabia inayomfanya afiti kwenye makala haya.

Isabela Mpanda

Katika mastaa micharuko, huyu yumo! Hajivuni, hajisikii lakini ukimchokoza lazima akushikishe adabu kwa matusi.

Posti zake zenye lugha chafu kwenye mtandao wa Instagram zipo nyingi lakini pia kwa wale wenye kumbukumbu watakumbuka kuwa staa huyu aliwahi kumtukana mwanamitindo Belina Mgeni na mpaka sasa hawaongei.

Hao ni baadhi ya mastaa ambao katika siku za hivi karibuni wameshika chati kwenye suala la kutukana mtandaoni.
LIST ya Mastaa wa BONGO Wanaongoza Kwa Kushusha Matusi Mtandaoni LIST ya Mastaa wa BONGO Wanaongoza Kwa Kushusha Matusi Mtandaoni Reviewed by Unknown on 3:00:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.