Lulu: Kuharibu ni Rahisi Kuliko Kujenga 'Habari za Ubaya Zinasambaa Sana Kuliko za Kujenga'

Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anasema baadhi ya watanzania wanapoteza muda wao katika mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuwaumiza wengine na kuwatusi bila sababu, huku wakiwa makini kusikiliza mabaya na kuyavumisha tofauti na taarifa njema zenye faraja kwa jamii.

“Ukiwa kama Binadamu kila jambo ukitaka kulisambaza kwanza tafakari katika nafsi yako, je huyo unayemtenda hana maumivu kama mwanadamu, tumekuwa mabingwa wa kuwaumiza wengine kupitia mitandao ya kijamii bila huruma,”


“Sijui kuna mtu anayeombea maumivu kila mara kwani iwe Lulu kila jambo baya, na asiwe mtu mwingine hiyo inaonyesha hata wanaojiita marafiki zangu waweza kuwa maadui zangu,”anasema Lulu.

Lulu anasema kuwa kuharibu ni rahisi sana kuliko kujenga kwani mara nyingi habari za kujenga ubaya zinasambaa sana kuliko wema, lakini anaamini kuwa Mungu ndio kila kitu na ajua ukweli wa kila jambo na hawezi kumhukumu mtu yoyote.
Lulu: Kuharibu ni Rahisi Kuliko Kujenga 'Habari za Ubaya Zinasambaa Sana Kuliko za Kujenga' Lulu: Kuharibu ni Rahisi Kuliko Kujenga 'Habari za Ubaya Zinasambaa Sana Kuliko za Kujenga' Reviewed by Unknown on 11:43:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.