Kadinda: Sipendi ‘Drama’ za Wema, Team Wema Msinitusi

Meneja wa staa mrembo, mjasiliamali na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu , Martin Kadinda ametoboa kuwa anapenda kila kitu kuhusu Wema isipokuwa ‘drama’ zake na kuwasihi watu ambao ni mashabiki na watetezi wa Wema Sepetu kwa kila jambo huko mtandaoni maarufu kama Team Wema wasimtukane .

Meneja huyo ambaye ni mbunifu wa mavazi aliyasema hayo hivi juzi kati kwenye ukursa wake mtandao mara baada ya kubandika picha ya Wema akiwa ndani ya ofisi ya Hospitali ya kimataifa ambayo imeingia mkataba na Wema kuwa Balozi wa hospital hiyo.

“Sichoki Kumwomba Mungu... Naamini ipo siku tutafika kileleni..... I love Every thing Abou tHer kasoro drama tu team wema msinitusi”- Kadinda aliandika.

Na kweli team Wema walimstahi meneja huyu.
Kadinda: Sipendi ‘Drama’ za Wema, Team Wema Msinitusi Kadinda: Sipendi ‘Drama’ za Wema, Team Wema Msinitusi Reviewed by Unknown on 12:53:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.