Baada ya Kupata Nafuu, Hili ndilo Neno la Shukrani Kutoka kwa Wastara


“Shukrani kwako uliyeniumba na ukanipa pumzi ya bule bila kukulipa chochote. Asante kwa wale wote wenye kuniombea mema na kunitakia mafanikio. Asante pia kwa wale wenye kuniombea mabaya mnanipa changamoto ambayo inanifanya nikaze buti kusaka mafanikio kwa kujua sio wote wanaonipenda nasio wote watalia leo nikianguka kimaisha au kufa asante kwa mnaonipa ushauri . Asante mnaonifariji naamini bila watu hakuna mtu mimi ni mtu nyinyi ni watu naendelea vyema na mtaendelea kupata huduma zangu za aina yeyote na nahitaji kuwapa mambo mazuri zaidi kisanaa na kibiashara kwa uwezo wa Mungu”- Wastara ameandika mtandaoni

Hivi majuzi Wastara alipata ajali ya gari aliyomsababishia majeraha madogo usoni.hivi sasa anaendelea vizuri zaidi.
Baada ya Kupata Nafuu, Hili ndilo Neno la Shukrani Kutoka kwa Wastara Baada ya Kupata Nafuu, Hili ndilo Neno la Shukrani Kutoka kwa Wastara Reviewed by Unknown on 11:45:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.